Jumanne, 19 Septemba 2017

Okwi akabidhiwa zawadi ya mchezaji Bora Mwezi Augosti



 Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ na klabu ya Simba, Emmanuel Arnold Okwi, amekabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni moja ambayo ni zawadi yake ya kuibuka mchezaji bora wa mwezi Agosti.

Mara baada ya kupokea mfano huo wa hundi Okwi amesema kuwa katika Ligi Kuu soka Tanzania Bara kuna wachezaji wengi ambao yeye kwa upande wake anavutiwa nao.

“Kwa Tanzania klabu nyingi zina wachezaji wazuri lakini nje ya Simba kuna mchezaji anaitwa Kamusoko ananivutia sana na Donald Ngoma pia”, amesema Emmanuel Okwi, ambaye amekuwa mchezaji bora wa mwezi Agost wa Vodacom Premier League ‘VPL’.

Maneno haya ameyasema Okwi baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Tsh 1,000,000 na Meneja Chapa wa Vodacom Tanzania, Yvonne Maruma na Afisa Udhamini, Ibrahim Kaude. Tuambie mchezaji unayemkubali zaidi kwenye ligi.

Hadi sasa Okwi anaongoza katika msimamo wa wafungaji mabao ya Ligi Kuu ya VPL msimu huu kwa kuwa na jumla ya mabao 6 , huku wanaomfuatia wakiwa na mabao mawili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni