Jumanne, 19 Septemba 2017

Noti za mamilioni ya pesa za’flashiwa’ chooni Uswisi,….kisa?



Waendesha mashtaka Uswisi wanachunguza tukio la noti nyingi za mamilioni ya pesa kukutwa zimechanwa na kudumbukizwa kwenye vyoo vya benki ya UBS na migahawa 3 inayoizunguka benki hiyo.
Noti hizo ambazo zilikua ni mpya kabisa na bado zilikua hazijaidhinishwa kuanza kutumika nchini humo zilikua ni za Euro 500 ambapo noti hiyo moja ya Euro 500 ni sawa na pesa za Kitanzania milioni moja na laki tatu (Tshs 1,300,000/=).
Imeelezwa kuwa nchini humo kuharibu pesa kwa makusudi sio kosa kisheria lakini waendesha mashtaka hao na jeshi la polisi wanataka kufahamu sababu haswa ya kutupwa kwa pesa hizo chooni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni