Jumanne, 19 Septemba 2017

Baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka 75, wafariki siku moja



Wanandoa waliodumu kwenye ndoa yao kwa miaka 75 George na Jean Spear ambao walikua wakiishi Uingereza wamefariki dunia siku moja kwa kupishana masaa machache tu kutokana na wawili hao kuugua ghafla.
George ambaye alikuwa mwanajeshi wa zamani nchini humo na Jean ambao wamesherehekea miaka yao 75 ya ndoa hivi karibuni waliugua ghafla ambapo Jean aliumwa ugonjwa wa ‘pneumonia’ na kulazwa hospitalini ambapo usiku wa siku hiyo hiyo George alilala usingizi mzito ambao uliishtua familia yake na ndipo walipoamua kumpeleka hospitali.
Siku hiyo hiyo saa 10:30 alfajiri Jean alifariki na kufuatiwa na George aliyefariki saa 4:45 asubuhi. Wawili hawa wakati wa uhai wao walijulikana kama ‘Maharusi wa Vita’ kwani walikutana na kufunga ndoa kipindi cha vita ya baridi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni