Jumanne, 19 Septemba 2017

BREAKING: Miili ya Watanzania 13 waliofariki ajalini Uganda imewasili



 Watu 13 wa familia moja waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea Uganda baada ya basi walilokuwa wanasafiria kutoka kwenye sherehe ya harusi kugongana na lori imefikishwa Tanzania na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Miili hiyo imepokelewa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na itapelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Lugalo na kesho September 20, 2017 itaagwa.
Watu hao walipata ajali September 17, 2017 majira ya saa 4:00 Usiku katika barabara ya Masaka, Uganda wakiwa njiani kurejea Tanzania wakiwa ni kutoka katika familia ya Naibu Waziri na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mpwapwa, Dodoma, Gregory Teu.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni