mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumatano, 13 Septemba 2017
Mwanamke avunja rekodi ya kufuga kucha kwa miaka 23 .duniani
Maajabu hayawezi kuisha duniani. Pale wanawake na mabinti wengine wanapohangaika kwa miaka mingi kufuga nywele zao ili ziwe ndefu, mwanamke Ayanna Williams wa Houston Texax, Marekani ameingia kwenye rekodi ya dunia ya mtu mwenye kucha ndefu zaidi za mikononi.
Ayanna ameeleza kuwa amezifuga kucha zake hizo kwa miaka 24 ambazo zinaripotiwa kuwa na urefu wa sentimita 576.4 na hii imemfanya awe na spidi ndogo sana katika kufanya mambo mbalimbali kwa kutumia mikono yake kutokana na urefu wa kucha zake lakini suala hilo halimsumbui.
“Nalipa watu wa kunisaidia kufanya kazi za ndani kwa sababu niko taratibu sana, na kazi nyingine siwezi kufanya kabisa kwa sababu ya urefu wa kucha zangu.” – Ayanna Williams.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni