Jumanne, 12 Septemba 2017

Inachopanga kufanya Liverpool baada ya Sadio Mane kufungiwa game tatu


 Baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayeichezea Liverpool Sadio Mane kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Man City uliyomalizika kwa Liverpool kupoteza kwa magoli 5-0, chama cha soka cha England FA kilimfungia Mane mechi.

 Sadio Mane alifungiwa mechi tatu baada ya kumchezea faulo mbaya golikipa Ederson iliyofanya imchane usoni na kushonwa nyuzi kadhaa katika jeraha hilo usoni, hata hivyo habari zilizoripotiwa leo ni kuwa Liverpool inajiandaa kukata rufaa kupinga urefu wa adhabu ya kufungiwa mechi tatu Sadio Mane kuwa ni kubwa.

 Kama Sadio Mane ataendelea kuitumikia adhabu hiyo ya mechi tatu, ina maana ataikosa michezo mitatu ya Liverpool wa September 15 dhidi ya Burnley, Leicester City na game dhidi ya Newcastle United.




 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni