Jumamosi, 19 Agosti 2017

WFP yawaenzi wahudumu wa misaada ya kiutu duniani



Wakati dunia ikishikamana Jumamosi Agosti 19 kuadhimisha siku ya usaidizi wa kiutu duniani mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP anaenzi mchango wa wahudumu wa kibinadamu kote ulimwenguni wakiwemo wafanyakazi wa WFP.
David Beasley amesema kila kona ya dunia wafanyakazi wa WFP wanafanya kazi usiku na mchana bila kuchoka kuhakikisha watoto na familia zao , wanaoteseka na kusambaratishwa na machafuko na vita wanapata mlo.
Amepongeza ujasiri wao na jitihada zao za kuwa msitari wa mbele kukabiliana na njaa hata wakati wa madhila, huku mara nyingi wakiwa katika hatari na wengine wamepoteza maisha yao.
Leo amewaenzi baadhi yao wakiwemo wahudumu watatu waliokuwa wakifanya kazi na WFP, Daniel James, Ecsa Tearp na Ali Elario, ambao waliuawa kwa kupigwa risasi mwezi aprili mjini Wau, nchini Sudan Kusini walikokuwa wakisambaza msaada wa chakula.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni