mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumanne, 22 Agosti 2017
Tundu Lissu kahojiwa kwa tuhuma za makosa mawili leo
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye alikamatwa na Polisi mapema leo wakati anatoka Mahakamani, amehojiwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya makosa mawili.
Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema, Tundu Lissu alihojiwa na Polisi kuhusiana na makosa mawili ambayo ni;
1. Kumkashifu Rais.
2. Uchochezi kuhusu kuzuiliwa na kushikiliwa kwa Ndege ya Serikali ya Bombardier.
Tundu Lissu anadaiwa kufanya makosa hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ijumaa iliyopita, August 18, 2017.
Aidha, Makene amesema, Lissu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, amekataa kutoa maelezo yoyote Polisi, akitumia haki yake ya kisheria kuwa mtuhumiwa ana haki, kisheria, kutaja jina na anuani yake tu anapokuwa anashikiliwa na Polisi hadi atakapofikishwa Mahakamani ambako ndiko atataoa maelezo kujibu mashtaka anayotuhumiwa nayo.
Lissu amesema yuko tayari kujibu mashtaka yake Mahakamani ambapo akiwa Polisi amepata msaada wa kisheria kutoka kwa Wakili Faraji Mangula, amb
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni