Jumamosi, 19 Agosti 2017

WANACHAMA SIMBA KUENDELEA KULISHWA ELIMU YA MABADILIKO LEO


 SEMINA za kuwaelimisha wanachama wa Simba juu ya mabadilko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo zinatarajiwa kuendelea Jumamosi.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Simba Hajji Sunday Manara amesema kwamba leo ni zamu ya wanachama wa wilaya za Ubungo, Kinondoni na Ilala ambao watakutana jengo la Ngawaiya liliopo Argentina, Manzese.
"Kwa wasiolifahamju jengo hilo ni kwamba lipo upande wa kushoto kama unaelekea Ubungo, katika barabara kuu ya Morogoro,"amesema. 
Manara amesema kwamba semina hizo zina lengo la kuwajengea uelewa mpana zaidi juu ya muundo mpya wa klabu, uliotokana na mabadiliko makubwa ya katiba yaliyofanywa na wanachama hao. 


Semina hiyo ya tarehe 19-8-2017, itaanza saa tisa alasiri kwenye jengo la Ngawaiya liliopo Manzese Argentina upande wa kushoto kama unaelekea Ubungo,katika Barabara kuu ya Morogoro,". 
Amesema pia Siku ya Jumapili kuanzia Saa 2:00 asubuhi, klabu itafanya Mkutano mkuu maalum wenye lengo hilo, ili taratibu za kuingia kwenye muundo mpya zianze kufanya kazi. 
"Mkutano huu muhimu na wa kihistoria, utafanyika pale pale tulipofanyia Mkutano mkuu wa kawaida wiki iliopita, Mwalimu Nyerere International Conference Centre uliopo maeneo ya Ocean road hapa jijini Dar es Salaam,". 
"Tunawaomba wana Simba popote walipo waje kuweka historia hii muhimu, historia itakayofanywa muandikwe kwa wino wa dhahabu, Historia ya kuitoa klabu ilipo na kuipeleka mbele zaid, kiuchumi, kibiashara, kimafanikio ya uwanjani, na pia kuwa klabu ya kwanza nchini kuingia katika muundo huu,unaokusudia kuifanya Simba iwe moja ya klabu bora kabisa Afrika.". 
"Niwaambie maandalizi ya Mkutano wa Jumapili ni kabambe na kila kitu kimekaa sawa, pengine kuliko Mkutano wa wiki iliopita," amesema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni