Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia
ametoa shukrani zake za dhati kwa wajumbe wote wa Mkutano Mkuu kwa kumpa
dhamana ya kuliongoza soka la Tanzania.
Karia pia amewataka wale wote waliyokuwa wakiwania nafasi mbali mbali
za uongozi ndani ya shirikisho hilo ambao kura zao hazikutosha katika
uchaguzi bado mawazo yao yanahitajika na kushirikiana kwa pamoja
kuhakikisha mchezo wa soka unakwenda mbele.
Kiongozi huyo wa ngazi za juu ndani ya Shirikisho lenye dhamana ya
kusimamia mchezo wa mpira wa miguu nchini amewapongeza pia viongozi
wenzake waliyofanikiwa kushinda na kuwaomba kushirikiana kwa pamoja
wakati huo huo akiwashukuru wadau, Serikali na taasisi zake bila ya
kuvisahau vyombo vya habari kwa ushirikiano wao katika kufanikisha zoezi
la uchaguzi kwenda salama hadi mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni