RUVU Shooting ya mkoani hapa, imesema kikosi cha Simba kilichocheza na
Rayon Sports ya Rwanda, Jumanne wiki hii, hakina uwezo wa kuwafunga
katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara Agosti 26, mwaka huu.
Katika Tamasha la Simba Day, Simba iliifunga Rayon bao 1-0 kwenye mchezo
wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau
Bwire alisema kama kuna mashabiki wanakiona kikosi cha Simba ni kizuri,
basi wamepotea kwani wao wanakiona cha kawaida kisichoweza kuwasumbua.
Bwire ametamba kuwa wataishushia kipigo kikali Simba watakapokutana
kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu itakayoanza Agosti 26, mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni