Ijumaa, 11 Agosti 2017

Mchezo wa Yanga na Ruvu Shooting wahamia Chamazi



 Mchezo wa kirafiki baina ya mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara klabu ya Dar es salaam Young Africans dhidi ya Ruvu Shooting iliyopangwa kuchezwa kesho Uwanja wa Taifa sasa utapigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.


Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa mchezo huo umehamishiwa Chamazi kutokana na Uwanja wa Taifa  kutarajiwa kutumika katika shukhuli za kiserikali siku ya Jumamosi

Baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting timu hiyo inatarajia kwenda Visiwani Zanzibar kwaajili ya kuweka kambi yake kabla ya kukutana na Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23 mwaka huu.
Viingilio vya mchezo huo sasa vitakuwa Sh7,000 kwa VIP na Sh5,000 mzunguko

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni