Jumanne, 1 Agosti 2017

Manara wa Simba amefunga mjadala wa Haruna Niyonzima leo

Related image

Baada ya habari  za muda mrefu kuhusiana na club ya Simba kuhusishwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Rwanda aliyekuwa anaichezea Yanga Haruna Niyonzima, kwa mara ya kwanza leo August 1 2017 Simba wamekubali na kuweka wazi.
Simba kupitia mkuu wao wa idara ya habari na mawasiliano Haji Manara wametangaza rasmi kumsajili Niyonzima ambaye bado yupo kwao Rwanda akimalizia mambo yake binafsi ya kifamilia na ataungana na timu Tanzania.
“Kuhusu Juuko ni mchezaji wetu na ataungana na timu suala la kwenda Orlando hatujapata taarifa, kuhusu Haruna ni mchezaji wa Simba ukiona ndege imetua hapa na wachezaji wa Simba ujue ndani yupo Haruna au anaweza kuja mapema kabla ya timu” >>> Manara


Image result for niyonzima imagesImage result for niyonzima images

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni