
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amepinga maamuzi ya Chama Cha Wananchi (CUF) kuwafukuza Uanachama Wabunge wawili wa chama hicho Magdalena Sakaya na Maftaha Nachuma na kusema Maalim Seif hatambuliki kama Katibu Mkuu wa CUF.
Msajili wa Vyama vya Siasa amesema hayo leo wakati akijibu barua iliyowasilishwa ofisini kwake na Katibu Mkuu wa (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad akimtaka msajili wa vyama kuwavua nafasi ya Ubunge viongozi hao.
Kufuatia
barau hiyo Msajili wa Vyama Vya Siasa amesema kuwa hamtambui Maalim
Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu wa CUF na kusema yeye anawatambua
Mwenyekiti wa CUF, Professa Ibrahim Lipumba pamoja na Magdalena Sakaya
kama mtu mwenye dhamana ya Katibu Mkuu wa CUF
Chama
Cha Wananchi (CUF) kipo katika mgogoro wa pande mbili upande wa Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif pamoja na upande wa Mwenyekiti wa CUF
anayetambuliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim
Lipumba, kufuatia mgogoro huo mpaka sasa kuna kesi mbalimbali ambazo
zimefunguliwa mahakamani kutokana na mvutano wa pande hizo zote mbili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni