Jumatano, 12 Julai 2017

Zaidi ya watu bilioni 2 hawana maji salama ya kunywa:WHO/UNICEF





Upatikanaji wa maji safi na salama bado ni changamoto katika nchi nyingi duniani.(Picha:UNIC/Tanzania)
Watu 3 kati ya 10 kote duniani au watu bilioni 2.1 ,wanakosa fursa ya kupata maji salama nyumbani na mara mbili yao hawana huduma za kujisafi, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la afya duniani WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa nyumba nyingi , vituo vya afya na shule pia havina sabuni na maji kwa ajili ya kunawa mikono.
Matokeo yake kila mwaka watoto 361,000 wa chini ya umri wa miaka mitano hufariki dunia kutokana na ugonjwa wa kuhara.
Usafi duni na maji machafu pia vinahusishwa na maradhi ya kuambukiza kama kipindupindu, kuhara damu, homa ya ini aina A na homa ya matumbo au typhoid.
Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa UNICEF Anthony Lake maji salama, huduma za kujisafi na usafi ni muhimu kwa ajili ya afya ya kila mtoto na kila jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni