Jumatano, 12 Julai 2017

Maeneo mapya 21 yaongezwa kwenye orodha ya UNESCO ya urith wa dunia




Eneo la urithi la Aphrodisias nchini Uturuki.(Picha:UNESCO)
Maeneo mapya 21 yameongezwa kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya urithi wa dunia na kufanya jumla ya maeneo ya urithi wa dunia kufikia zaidi ya 1000.
Tangazo hilo limetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO wakati wa kufunga mkutano wa 41 wa kila mwaka wa kamati ya urithi wa dunia uliokuwa ukifanyika mjini Krakow Poland.
Kamati hiyo hukutana maramoja kwa mwaka kuamua ni maeneo gani ya kitamaduni na kihistoria yenye thamani ya kimataifa yanastahili kuingia kwenye orodha ya urithi wa dunia pamoja na yale yanayohitaji kulindwa.
Angola na Eritrea wameshuhudia kwa mara ya kwanza maeneo yao yakiingia katika orodha hiyo.
Wakati huohuo kituo cha kihistiria cha Vienna kimejumuishwa katika orodha ya urithi wa dunia ulio hatarini, huku maeneo matatu yaliyokuwa kwenye orodha hiyo awali yakienguliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni