Jumatano, 12 Julai 2017

Askari wa UNMISS wasitisha jaribio la utekaji nyara kwa wakimbizi




Walinda amani wakipiga doria nchini Sudan Kusini.(Picha:Isaac Billy/ UNMISS)
Nchini Sudan Kusini, askari wawili waliovaa sare za kijeshi na kubeba silaha walijaribu kuwateka nyara wakimbizi watatu karibu na kituo cha ulinzi wa raia cha Bentiu kinacholindwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS. Taarifa kamili na Amina Hassan.
(Taarifa ya Amina)
Askari hao wanaodhaniwa kuwa ni wa SPLA waliwakaribia na kuanza kuwanyanyasa wakimbizi watano au sita ambao walikuwa wakilima mashamba yao na kujaribu kuwateka nyara watatu na ndipo askari wa ulinzi wa amani wa UNMISS kutoka Mongolia walipojaribu kuingilia kati na baada ya mjadala mkali askari wa SPLA wakakimbilia vichakani na kuanza kufyatua risasi.
Kufuatia ghasia kubwa za Julai 2016 zilizolazimu Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa UNMISS haikuwajibika ipasavyo kuwalinda raia, na matokeo yake kuweka mapendekezo ya utekelezaji wakati wa ghasia, Naibu Kamanda wa Sekta ya Kaskazini ya Bentiu, Kanali Gaurav Bagga amesema wanajeshi wake walichukua tahadhari kubwa kabla ya kurejesha mashambulizi..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni