Mtaaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Ikponwosa Ero anafanya ziara yake ya kwanza nchini Tanzania wiki ijayo kuanzia Juali 18-28, ili kutathimini hali ya haki za binadamu za watu wenye ulemavu wa ngozi au albino.
Bi Ero amesema ziara hiyo ni muhimu sana ukizingatia kwamba kumeripotiwa mashambulizi mengi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania, na hatua za kipekee ambazo zinachukuliwa na serikali ya nchi hiyo kushughulikia ukatili huo.
Ero ambaye atazuru kwa mwaliko maalumu wa serikal, atatathimini pia utekelezaji wa hatua hizo, kubaini mapungufu na kuona uwezekano wa kuziba mapengo hayo.
Tanzania ni moja ya nchi za kwanza kuripotiwa kutokea mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ikiwemo mauaji, kutekwa na kukatwa viungo kwa ajili ya masuala ya ushirikina.
Ni takribani muongo mmoja tangu kuripotiwa shambulio la kwanza dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, hivyo mtaalamu huyo pia ataangalia ni ulinzi wa aina gani wanapewa wale wanaohofia maisha yao ikiwemo makazi ya muda, na kudodosa ukiukwaji wa aina zote wa haki za watu hao ikiwemo ukatili, kuishi kwa hofu, na kusahaulika katika malengo ya maendeleo endelevu.
Mwisho wa ziara yake atazungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam na
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni