
Duniani yapo mengi ambayo yanavuta
hisia ukiyasikia. Wengi wetu huamini kuwa umeme umekuwa ukizalishwa kutoka
katika vyanzo mbalimbali kama mashine, betri, jua na maji.
Lakini amini au usiamini kuna viumbe
ambao wanazalisha umeme mwingi wenye nguvu hata ya kuweza kumuua binadam mtu
mzima ndani ya sekunde.
Moja ya viumbe wenye uwezo wa
kuzalisha umeme ni samaki aina ya electric eel au electricus fish
ambae ana umbo refu mfano wa bomba huwa akikuwa anaweza akafikia urefu wa mita
2 ( futi 6-7) na uzito wa kilo 20 kitu kinachomfanya kuwa samaki mkubwa katika
kundi la Gymnotiformes.
Samaki huyu
ana rangi ya kahawia iliyokolea kwa upande wa nyuma(mgongoni) na rangi ya manjano
au machungwa mbavuni na tumboni. Ana mdomo wenye pembe ambapo pembe hiyo hujitokeza mwishoni mwa pua.
Kama walivyo samaki wa kundi la ostariophysan, kibofu cha kuogelea kimegawanyika sehemu mbili,
ndani ambapo kimeungana na sikio landani kwa kutumia mtililiko wa vifupa
ambavyo vinatokea kwenye uti wa shingo ambao kitaalam unaitwa Weberian apparatus,
ambao ndio unaomsaidia kupata uwezo wa kusikia.
Sehemu ya pili ni ile inayoanzia
nyuma kuja mbele na inachukua karibu sehemu yote ya urefu wake na ndio
inayomsaidia kuweza kuelea ndani ya maji. Samaki huyu ni lazima aje juu ya maji
kila baada ya dakika kumi kupata hewa(kupumua) kabla ya kuludi chini ya maji. Karibia
asimia 80 ya hewa ya oxygen anayoivuta anaipata kwa njia hii.
Electric eel ana viungo tofauti
vinavyomsaidia kuzalisha umeme, cha kwanza kinazlisha umeme kwa ajili ya kuwindia
na kingine kinazalisha kwa ajili kusikilizia. Viungo hivi vya kuzalishia umeme
vinatengeneza 4/5 ya mwili wake wote, na vinmuwezesha kuzalisha umeme wa aina
mbili ule wenye nguvu kubwa na ule wa nguvu ndogo. Viungo hivi ambavyo
vimeundwa na elektroliti
vimejipanga kwa pamoja ambapo ngunvu ya umeme inapita kama vile ufanyavyo
kwenye waya.
Kipindi eel
anapohisi windo ubongo wake hutuma taarifa kwenye elektroliti na hii hupelekea
kufungua chaneli ya madini yachuma ambayo inaruhusu sodium kupita kwa kubadili
mkondo kuludi nyuma ambapo mabadiliko ya haraka hutokea katika mkondo na
kupelekea kuzalisha umeme kama vile betri ambapo seli hupangwa pamoja ili
kupata umeme.
Ndani ya electric eel, baadhi ya seli 5,000 mpaka 6,000 zilizojipannga kwa
pamoja ambazo zina uwezo wa kuzalisha volt 860 na watt 860 ndani ya chini ya
sekunde moja. Umeme huu una uwezo wa kumdhuru hata kumuua mtu mzima.
Pia ndani ya smaki huyu kuna ogani nyingine
ijulikanyo kama Sach’s ambayo inaundwa na seli nyingi ambapo kila seli
inazalisha umeme mdogo wa volti 0.5, organi hii inazalisha umemewa 10V katika mawimbi ya 25hHz kwenda juu
, ambapo huutumia umeme huu mdogo kwa ajili ya kufanya mawindo yake hasa
ukizingatia kuwa hana macho.
Pindi samaki huyu anapojihakikishia kuwa windo lake
lipo ndani ya mzio wake basi huachia ule umeme mkubwa ambapo ukimpata windo
basi hupoteza nguvu na hivyo kumezwa na samaki huyu.
Electric eels amekuwa akifanyiwa
uchunguzi wa bioelectrogenesis. Na
amekuwa ni kivutio kwa watafiti, ambapo watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani na wizara ya taifa ya
teknolojia wanajalibu kuona kama wanaweza kutengeneza seli feki zinazofanana na
za samaki huyu au kuboresha seli za samaki huyu. Uzalishaji ama uboreshaji wa
seli hizo unaweza kuendelezwa kisayansi ili kuweza kuwa kama chanzo cha nguvu
kwa viungo vya vya bandia na vifaa tiba.
Electric eels anaishi katika maji ya
baridi(yasiokuwa na chumvi) katika msitu wa Amazon na katika
bonde la mto Orinoco huko America kusini. Na maranyingi hupatikana
katika kina cha mto katika maji yaliyotulia kiasi.
Chakula chake kikubwa ni wadudu,
konokono, kaa, minyoo ingawa mala nyingine anaweza kula samaki na wanyama
wadogo wadogo kama panya.
Uzalialianaji wake ni wa kutaga
mayai kipindi cha kiangazi ambapo hutaga mayai karibia 3000. Samaki jike ndio
mwenye umbo dogo kuliko dume.

chanzo vyote blog .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni