Alhamisi, 22 Juni 2017

MJUE NUNGUNUNGU


 



Jioni moja nikiwa nimeboreka nikaona itakuwa vema ikiwa nitafanya kutoka na kwenda kutembea tembea hapa na pale, kwakua makazi yangu yamejitenga na makazi mengine kwa kiasi kikubwa basi ni lazima ukatize kwenye vichaka vya hapa na pale, mbele yangu nikamuona mnyama mdogo mdogo akikatiza kama ananusanusa chini lakini kwa haraka…ikanibidi kusimama ili kuona kinachoendelea, kwanza niliona kama sungura au panya mkubwa na kwa jinsi nnavyoipenda nyama pori nikajisemea mboga ya jioni ya leo imejileta kirahisi namna hii hapa ni mwendo wa chui nakula mboga. Alivyojichomeka kichakani na kwa kuwa kicha kile nakifahamu vema sikupoteza muda nipo pale na gongo langu mkononi, la haula kwa karibu nikagundua nimekosea timing maana naweza kuwa windo la myama huyu…maana kumekuwepo na hadidhi kadhaa za kumhusu mnyama huyu maalufu kama nungunungu, asije nirushia mishale yake nikapoteza macho yangu huku bado nayapenda.
Lakini niashangaza na kuwa pamoja na kuniona hakuwa na shida na mimi wala hakulusha miba yake na badala yake kwa mwendo uleule akaingia shimoni  na sikumuona tena, nikabaki kuwaza kupo wapi kule kulusha miba mbona ni mpole hana madhara kwa binadamu…kutokea hapo nikatamani kumjua huyu kiumbe ni wa namna gani?


Nungnungu au nungu ni ni mnyama mgugunaji mwenye ngozi yenye miiba iliyochongoka wanayotumia kujilinda na maadui,Ila sio kwa kuilusha miiba hiyo. Mnyama huyu mdogo anayeishi milimani, mashambani, na msituni ni wa kipekee sana. Ana manyoya magumu ya kahawia na meupe kichwani na shingoni, lakini miiba yake yenye ncha za rangi ya manjano ndiyo humtambulisha zaidi. Miiba hiyo yenye urefu wa sentimeta mbili hivi ni mikali na imepangwa katika makundi-makundi.
 Miiba ya kila kundi hukua kutoka mahali pamoja na kuufunika mwili wake. Kila mwiba umezungukwa na mitaro-mitaro na umejipinda mahali ambapo umeshikamana na ngozi na kufanyiza pembe-mraba. Mwiba huanza kuwa mwembamba na kujipinda unapokaribia kushikana na ngozi. Ndiyo sababu nungunungu hawezi kuchomwa na miiba yake hata akianguka kutoka mahali palipoinuka. Ama kweli, nungunungu ameumbwa kwa njia ya ajabu!
    Ni vigumu sana kuweza kumuona kwa vile anaishi kwa mashaka sana,maana mara tu anapoonekana machoni pa watu hushambuliwa na kuwaua kwa sababu mbalimbali.Wengine huwaua kwa sababu ya kuwatuhumu kuwa wanakula mazao yao mashambani.Lakini wengine humuua kwa sababu wanadai kuwa miiba yake ni dawa. Nungunungu hupenda kuishi na kufurahia mazingira yenye mapori na misitu ili kujihadhali na ukatilii anaotendewa. Hupenda  sehemu zenye nyasi ndefu ndefu ajili ya usalama wake.
 
  Anaposhtuliwa, nungunungu hujikinga kwa kujikunja kama mpira. Misuli yake yenye nguvu hukaza ngozi yake yenye miiba na kuufunika mwili wake mzima. Ngozi hiyo yenye miiba hufunika kichwa, mkia, miguu, na sehemu zake za chini. Mnyama huyo anaweza kujikunja hivyo kwa muda mrefu.
   Nungunungu huona njaa wakati wa jioni. Chakula chake cha jioni huwa wadudu na minyoo, lakini wakati mwingine anaweza kula panya, chura, mjusi, au hata njugu na matunda ya beri. Nungunungu husikia vizuri sana. Pia ana uwezo wa kunusa wenye nguvu, na unaweza kutambua jambo hilo ukiona pua lake refu lenye umajimaji.
  Mbali na mbweha na melesi, nungunungu hana maadui wengi mwituni. Melesi aweza kubambua ngozi ya nungunungu kwa kucha zake zenye nguvu bila kuumizwa na miiba. Nimewahi kuona ngozi ya nungunungu mara kadhaa. Huenda ngozi hiyo ikawa imebaki baada ya melesi kumla nungunungu mzima. Kwa upande mwingine, mbweha hawezi kustahimili miiba ya nungunungu, lakini anaweza kujaribu kumviringisha hadi majini, ambapo nungunungu hulazimika kujikunjua la sivyo atakufa maji. Kwa kuwa nungunungu ni mwogeleaji hodari, huenda akafikia mawe au kuingia ndani ya mashimo yaliyo kando ya mto kabla mbweha hajamnyakua na kumfanya kuwa kitoweo chake.
Nungunungu huanza kujamiiana katikati ya miezi ya Mei na Julai, na wanarudia kufanya hivyo kwa mara ya pili katika kipindi hichohicho. Baada ya majuma manne hadi sita, watoto watatu au wanne huzaliwa wakiwa na uzito unaopungua gramu 30. Watoto hao huwa hawaoni wala kusikia wanapozaliwa, hivyo wanaweza kushambuliwa kwa urahisi katika majuma mawili ya kwanza. Kisha miiba humea mahali palipokuwa na manyoya laini. Baadaye wanaweza kujikunja kabisa. Kabla ya kupata uwezo huo, wao huruka juu mara moja na kutoa mlio mkali wa kuchatachata wanaposhtuliwa. Jambo hilo huwashtua maadui zao wengi.
Wakati nungunungu amelala, yeye hutumia mafuta aliyohifadhi mwilini katika miezi ya joto. Wakati huo joto la mwili wake hupungua sana, naye hupumua kidogo sana hivi kwamba si rahisi kutambua kama anapumua. Ana tezi maalumu anayotumia kudhibiti hali ya joto la mwili wake anapolala. Kiasi cha joto kikipungua sana wakati huo, tezi hiyo hutokeza joto zaidi linalomfanya ajue kwamba anapaswa kutafuta makao yenye joto zaidi, yaliyozingirwa zaidi. Hii haimaanishi kwamba wakati wa baridi nungunungu hana habari kuhusu kinachoendelea katika mazingira yake. Anaweza kusikia sauti yoyote iliyo karibu naye, na kumfanya asonge kidogo.

Ukijaribu kumfuga nungunungu, yeye hupanda ukutani, au kwenye bomba la maji na kuponyoka kwani anapenda kulisha katika eneo kubwa. Ndiyo sababu, si rahisi kumfuga au kumfanya awe mnyama kipenzi. Ni vizuri zaidi kwamba hafugwi kwa kuwa yeye hubeba viroboto wengi sana
chanzo mtandao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni