Albamu hiyo iliyochota vionjo tele vya kabila la Kihaya, mashabiki wengi waliipachika jina la ‘Chambua kama Karanga’ kutokana na maneno yanayopatikana katika wimbo wa Maria Salome ambao umebeba jina la albamu.
Inaelezwa miezi mitatu baada ya kutoa albamu hiyo, Saida Karoli alipata mwaliko wa kuimba nchini Uganda ambapo Kabaka wa Buganda alimwalika katika sherehe ya kiutamaduni, pia kumfanya kuwa mwanamuziki wa mwaka katika sherehe hiyo.
Pia albamu hiyo ilifuatiwa na ziara kubwa alizofanya katika nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya ambapo alipata mafanikio makubwa na Saida kujikuta akibatizwa na kupewa jina la malkia wa nyimbo za asili.
Karibu Diamond, Darassa na Belle 9
Septemba 18 mwaka jana Diamond Platnumz alitoa wimbo uitwao Salome akiwa amemshirikisha Rayvanny. Wimbo ukiwa umekopa beat, melody na baadhi ya maneno kutoka kwenye wimbo wa Maria Salome wa Saida Karoli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni