Jumatatu, 26 Juni 2017

OKWI RASMI MSIMBAZI



Good news kwa mashabiki wa Simba SC imetangazwa , baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emanuel Okwi, imeripotiwa kuwa Okwi amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili hivyo ni rasmi amerejea Simba.
Usajili wa mshambuliaji huyo raia wa Uganda ambaye amejijengea jina na mashabiki wengi Tanzania, umekamilishwa na mlezi wa Simba na mfanyabiashara mkubwa Mohamed Dewji ambaye jarida la Forbes linamtaja kuwa ni bilionea wa 16 Afrika.


Kama utakuwa unakumbuka vizuri hii sio mara ya kwanza kwa Emanuel Okwi kuichezea Simba, aliwahi kuichezea kwa mara mbili kabla ya leo kujiunga nayo tena kwa mara ya tatu, mara ya kwanza ilikuwa 2010-2013 akauzwa kwenda Etoile du Sahel ya Tunisia.
Mara ya pili 2014-2015 akitokea Yanga na aliuzwa tena kwenda SønderjyskE ya Denmark ambapo alikosa nafasi ya kucheza na kuamua kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili na kurejea kwao Uganda katika club yake ya zamani ya SC Villa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni