
Mashirika yasiyokuwa ya serikali
nchini Tanzania yameonywa dhidi ya kuendesha kampeni kutaka wasichana
walio na watoto kuruhusiwa kurudi shuleni.
Waziri wa mambo ya
ndani Mwigulu Nchemba, ametishia kuyapokonya vibali vya usajili
mashirika hayo kwa mujibu wa gazeti la Citizen.Hii ni baada ya Rais John Magufuli kuuambia mkutano wa hadhara kuwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania wasichana wajawazito hawewezi kurudi shuleni,
Magufuli alisema: "Baada ya kufanya hesabu kidogo, atakuwa akimuomba ruhusa mwalimu kuenda kumnyonyesha mtoto anayelia.
chanzo na bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni