Jumanne, 27 Juni 2017

WANAWAKE WAWEKA REKODI YA KUCHEZA SOKA KATIKA KILELE CHA UHURU, MLIMAKILIMANJARO




Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari .
 
Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) ,Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .

Jina ZUZU Lamkera Mizengo Pinda


WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amesema anafarijika kuona mchakato wa kubadilisha jina la kijiji cha Zuzu umeanza kwa kuwa jina hilo halina ustaarabu kulingana na maana yake halisi.

Alisema sasa wanakwenda kupata jina linaloendana na eneo hilo ambalo wanaishi wachapakazi wengi. Shamba la Pinda lililoko kijiji cha Zuzu ni moja ya miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru juzi na kuwawezesha wakimbiza Mwenge kitaifa kushuhudia shughuli mbalimbali zinazofanyika katika shamba hilo ambalo pia linatajwa kuwa shamba darasa kwa sasa.

Alisema licha ya mafanikio mengi ambayo yamepatikana kilio chake ni jina la kijiji kuwa halina ustaarabu masikioni mwa watu. 
”Zuzu maana yake ni mpumbavu, silipendi jina hilo, sijui walitoa wapi nimekwenda kwenye mtandao nakuta jina ni Zinje kila nikiuliza sipati jibu lini walitubaini sisi ni mazuzu watu wazuri huku tunafanya kazi tunajiendeshea maisha yetu,” alisema 
“Nikamwambia mkuu wa mkoa jina hili si letu ila wametubambikiza tu. Hoja tunayo nadhani serikali imetusikia na tutapata jina ambalo linaendana na eneo hili,” alisema.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, Amour Hamad Amour amewataka viongozi nchini kutekeleza kwa vitendo sera, mipango na mikakati ya kukuza uchumi badala ya kuhubiri na kuhimiza kwa wananchi bila wao kuonesha mfano. 
“Huu ni mfano ulio bora unaopaswa kuigwa na kila kiongozi mikakati ya kukuza uchumi katika nchi inatakiwa kutekelezwa kwa vitendo,” alisema.

Awali akitoa maelezo kuhusu shamba hilo, mke wa Waziri Mkuu mstaafu Pinda, Tunu Pinda alisema harakati za kuanzisha shamba hilo zilianza mwaka 2001 na shamba hilo lina ukubwa wa ekari 60. 
Alisema shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika shamba hilo ikiwemo kilimo, ufugaji na huzalisha gesi ya asili ya biogas kwa ajili ya nishati ya kupikia na taa.

Alisema shamba hilo limekuwa likitumia mbolea ya samadi katika kilimo. Pia alisema shamba hilo lina mizinga 403 ya kisasa ambapo katika msimu wa mavuno uliopita kiasi cha tani 7.5 za asali zilipatikana. ‘’Bidhaa zinapatikana dukani kwa nembo ya Pinda Honey” alisema



Kauli ya CHADEMA Baada ya Lowassa Kuitwa Polisi Leo Kwa Mahojiano





Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano.

Mhe. Lowassa ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia CHADEMA, kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.

Tayari Chama kimetoa maelekezo kwa Kurugenzi ya Katiba na Sheria ya Chama kuhakikisha kuwa Mhe. Lowassa anapata msaada wa kisheria wakati wa mahojiano hayo.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Mhe. Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari pamoja na Watanzania wenzetu Waislam waliokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambapo amekuwa kiitaka Serikali kuzingatia misingi ya utawala bora kama mojawapo ya misingi muhimu ya kuendesha nchi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Watanzania wote.

Imetolewa  Jumatatu, Juni 26, 2017 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Francis Cheka afunguka mazito baada ya kutwangwa na Mswisi



 Baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Mswisi Enes Zecirevic usiku wa kuamkia leo Jumapili, bondia Francis Cheka amefunguka sababu za kupoteza pambano hilo.


Cheka ambaye alipigwa kwa pointi za majaji 3-0 kwenye pambano hilo la raundi nane la uzani mwepesi wa juu (kg 81) lililofanyika mjini Geneva, amesema pambano hilo alishindwa kwa pointi za ugenini kwani ilitakiwa ashinde kwa Knock Out.
Nisingeweza kushinda kwa pointi, nilijua matokeo yale baada ya kumaliza raundi zote. Siku zote unapocheza ugenini na kumaliza raundi zote ni vigumu kupewa ushindi dhidi ya mwenyeji, ndivyo ilivyokuwa hata na kwangu.
“Nimeumizwa kuharibu rekodi yangu, lakini sijashangazwa na kupigwa kwa pointi kwani ni ushindi ambao yoyote anaweza kupewa,” amesema Cheka kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi.





 


 

RAIS MSTAAFU ALHAJI HASSAN MWINYI AWAONGOZA WAISLAMU KATIKA SWALA YA EID ELFITR JIJINI DAR LEO




RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM




PICHA NA IKULU TAREHE 26.6.2017

Waliomuingiza mtu mweusi kwenye jeneza, Mahakamani Afrika Kusini



 Hatimaye wakulima wawili weupe wanatarajiwa kufikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini, kwa tuhuma za kumsukuma mtu mmoja mweusi na kumuingiza ndani ya jeneza, huku wakitishia kummwagia mafuta ya petroli ili kumteketeza kwa moto akiwa hai.

Washtakiwa hao Willem Oosthuizen na Theo Jackson, walikamatwa Novemba mwaka jana, baada ya video ya kitendo hicho kuzungushwa mitandaoni.

Walisema kuwa, Victor Mlotshwa alipita kwenye shamba lao lililopo katika jimbo la Mpumalanga, bila ya kuwa na idhini, na kwamba hatua waliyochukuwa ilikuwa ni kumuadhibu.
Katika kusikilizwa kwa kesi hiyo awali, Jaji wa mahakama alisema kuwa wakulima hao walikuwa ni wakatili na waliojaa tabia za ubaguzi wa rangi.

Nyuki ‘wamlazimisha’ mshukiwa kujisalimisha Kenya

Taarifa kutoka magharibi mwa Kenya zinasema kuwa mtuhumiwa wa wizi wa gari alijisalimisha kwa polisi Related imagebaada ya kuvamiwa na nyuki akiliendesha gari hilo.


Mwandishi wa BBC, Wanyama wa Chebusiri kutoka Nairobi, anasema ripoti hiyo iliyoripotiwa mara ya

 kwanza kwenye gazeti la The Star la nchini Kenya, imewaacha wengi vinywa wazi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwenye gari aliamini kwamba mshukiwa alimuwekea dawa ya kulevya kwenye kinywaji katika hoteli moja na kumfanya apoteze fahamu.

Saa kadha baada ya kurejelewa na fahamu, alipata gari lake halipo.
Mwenye gari alitafuta msaada wa mganga wa kienyeji ambaye alimhakikishia kwamba mtuhumiwa atavamiwa na nyuki kabla ya kuondoka katika mji wa Bungoma ulioko magharibi mwa Kenya.

Punde si punde, nyuki walimvamia mshukiwa akiwa ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara moja maarufu mjini Bungoma.

Katika harakati za kutaka kujinusuru kutoka kwa makali ya nyuki, mshukiwa alichana mbuga akielekea kituo cha polisi cha Bungoma, huku akipiga kelele za niokoe lakini wapi, nyuki walikuwa naye 'hapa kwa hapa'.

Mwanamme huyo alijaribu kutoka katika kituo cha polisi lakini nyuki walimwandama unyonunyo kabla ya polisi kumuokoa kwa kumfungia ndani ya seli kwa mahojiano.

Mkuu wa polisi katika eneo la Bungoma David Kirui ameiambia BBC kwamba nyuki walikuwa wamezingira kituo hicho cha usalama huku mshukiwa akiwa anahojiwa kwa madai ya wizi wa gari.

Kisa hiki cha nadra kiliwastajabisha na kuwashangaza wakaazi wengi wakiachwa vinywa wazi, huku wengi wa kijiuliza, je, ushirikina ungalipo?
CHANZO BBC

Wanawake 'wacheza utupu' watumbuiza wafungwa Afrika Kusini



 Wafungwa katika gereza la Sun City nchini Afrika Kusini, walitumbuizwa na 'wacheza utupu' kama sehemu ya hafla rasmi.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha wanawake wawili waliovalia nusu uchi wakiwaburudisha wafungwa katika jela hiyo mjini Johannesburg.

Idara ya huduma ya kurekebisha watu tabia imethibitisha kwamba kisa hicho kinachoonyesha picha za mahabusi wakiwa wamekumbatiana na akina dada ni kisa cha ukweli kilichotokea katika jela.
Uchunguzi kamili umeanzishwa, afisa wa idara ya magereza James Smalberger ameambia wanahabri.

"Hatuwezi kuvumilia yale ambayo tumeyaona katika mitandao ya kijamii tangu Jumamosi," Bw Smalberger, ambaye ni kaimu kamishna wa idara ya taifa ya magereza amesema.

Askari jela 13 wamesimamishwa kazi na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na sheria za idara hiyo.

Hafla hiyo iliyoandaliwa 21 Juni ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Vijana, ambayo ni sehemu ya mpango unaokusudiwa kuwarekebisha tabia wafungwa.

Lakini wanawake hao - na mavazi yao - waliwashangaza maafisa.
Msemaji wa idara ya magereza ya Gauteng Ofentse Morwane aliambia TimesLive: "Wanenguaji viuno walifika, tuliona walikuwa wanavalia nguo za ndani. Waliandaa igizo kama la kuvua nguo hivi na wahalifu hao."

Picha za wanawake hao wakiwaburudisha wafungwa zilianza kusambaa mitandao ya kijamii wikendi, na kusababisha uvumi kwamba huenda labda maisha ni mazuri gerezani kuliko nje ya jela.

Kuna wengine katika mitandao ya kijamii ambao wana hasira kwamba hafla hiyo iliruhusiwa kuendelea.

Bw Smalberger amesema hakuna pesa zozote za 'mlipa kodi' zilizotumiwa kuwalipa wanawake hao.
Anasema wanawake hao waliingizwa ndani ya jela na mtoaji huduma kutoka nje.

Korea Kaskazini yakataa pendekezo la kushirikiana Olimpiki

2018 PyeongChang Januari 26, 2016


Korea Kaskazini imekataa ombi kutoka kwa Korea Kusini kwamba nchi hizo mbili ziunde timu moja kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi mwaka ujao.
Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in alikuwa ameunga mkono ushirikiano huo ambao ulipendekezwa na waziri wa michezo Do Jong-hwan.
Lakini mwanachama wa Kamati ya Olimpiki ya Korea Kaskazini (IOC) Chang Un amepuuzilia mbali wazo hilo - na kusema kwamba huu si wakati wa kushauriana kuhusu maafikiano.
Michezo hiyo katika Pyeongchang, Korea Kusini itafanyika kuanzia 9-25 Februari

 Mataifa hayo mawili yamewahi kushirikiana na kuunda timu moja awali - katika mashindano ya ubingwa wa tenisi ya mezani duniani mwaka 1991.
Lakini Bw Chang ameambia vyombo vya habari Korea Kaskazini kwamba: "Ilituchukua vikao 22 vya mazungumzo kuunda timu moja wakati huo...ilituchukua miezi mitano."
"Huo ndio uhalisia tunaokabiliana nao."

Rio de Janeiro, Brazil, August 2016
Waziri wa michezo wa Korea Kusini alikuwa amependekeza kwamba mataifa hayo yanaweza hata kuunda timu ya pamoja na mchezo wa magongo wa kuteleza kwenye barafu, na hata akapendekeza Kaskazini iwe mwenyeji wa mashindano ya kuteleza kwenye barafu ili kufanya michezo hiyo kuwa michezo ya Olimpiki ya amani.
Rais Moon, hutetea kuwepo kwa mazungumzo na Pyongyang, naye aliunga mkono wazo la ushirikiano zaidi katika Olimpiki.
CHANZO NA BBC

Rayvanny akamilisha ndoto yake kwa Jason Derulo



 Kushindwa kutumia fursa kwa kila nafasi unayoipata imeonekana ni dhambi kubwa kwa wasanii wa WCB. Hatimaye Rayvanny amekamilisha ndoto yake aliokuwa akiiota kwa muda mrefu.
 
 Hitmaker huyo wa Zezeta, ambaye siku chache zilizopita alinyakuwa tuzo ya BET, amefanikiwa kukamilisha kufanya kazi na Jason Derulo kutoka Marekani.
Kupitia mtandao wa Instagram, Ray ameweka picha akiwa syudio na msanii huyo na kuandika, “God bless you my brother @jasonderulo its amaizing opportunity,am so grateful for that……… Toka Saa 8 Usiku amekaa na mimi hadi Asubui… Studio kulikua na Watoto wakaaaaaliiiii lakini kawacha waondoke sababu walichoka kukaa studio yeye kabaki na sisi tu. Naamini kilichofanyika Mtakipenda. Thanks boss @afrikidd @babutale.”
Baada ya wasanii hao kukamilisha kazi yao hiyo walijumuika pamoja katika kucheza mchezo wa mpira wa kikapu ambapo Ray alijikuta akiambulia za uso kutoka kwa Jason. Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana nchini Kenya kwenye Coke Studio Afrika wiki chache zilizopita.

chanzo na bongo 5 .

LOWASSA AITWA NA MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI [DCI]

Image result for lowassa images

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa amepata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kesho Jumanne, saa 4 asubuhi kwa ajili ya mahojiano. Taarifa iliyotolewa na CHADEMA imesema kuwa  hajapewa maelezo wala ufafanuzi wowote kuwa mahojiano hayo yatahusu nini hasa.
CHADEMA wameeleza kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa mahojiano hayo yanahusishwa na kauli za Lowassa alizotoa katika nyakati tofauti hivi karibuni wakati akishiriki futari katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kwenye vyombo vya habari leo Lowassa ameripotiwa akimtaka Rais Magufuli kuwaachia huru mashehe wa uamsho ambao inadaiwa wanashikiliwa kwa miaka minne sasa.

Jumatatu, 26 Juni 2017

UTANI WA WABONGO



baada ya kuwepo  kwa zuio la kutotumia jina la mcheza soka, raia wa  kenya victor wanyama ,katika mtaa mojawapo jijini Dar es salaam .kumeibuka utani wa kuandika majina ya baadhi ya wadau wa soka hapa nchni kwenye mabango ya mtaa.