mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania
blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla
kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Polisi mkoani hapa wanamsaka mwanamke ambaye aliyejifanya muuguzi na
kuiba mtoto wa kike wa siku moja kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali
ya Mkoa wa Mbeya.
Mtoto huyo alizaliwa kwa njia ya upasuaji na Sarah Mwasanga (40), mkazi wa Iganzo jijini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mpinga alisema tukio hilo
lilitokea juzi alfajiri kabla ya ndugu na jamaa kuingia kuona wagonjwa.
Mpinga alisema mwanamke huyo alifika hospitalini hapo kwa pikipiki huku
akiwa amebeba kitu mithili ya mtoto na alipohijiwa na walinzi getini,
alieleza ana mgonjwa ameandikiwa sindano za masaa hivyo akaruhusiwa
kuingia.
“Alitumia mbinu ambayo kwa namna moja au nyingine ilifanikisha azma yake
jambo ambalo hata wakati anatoka walinzi hawakumtilia shaka kwa
kutambua tayari kapatiwa huduma,” alisema.
Mpinga alisema awali alipoingia kwenye wodi ya wazazi, aliwahoji
kinamama waliojifungua kuwa anahitaji mtoto wa kike kwa ajili ya
kumpatia chanjo, ndipo mzazi wa mtoto huyo alimkabidhi kwa kutambua ni
muuguzi kutokana na mavazi aliyokuwa amevaa.
Alisema hilo ni tukio kubwa lililotokea mkoani hapa tangu aliporipoti na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Yahaya Msuya amekiri kutokea kwa tukio hilo, na kwamba kwa sasa lipo kwenye uchunguzi zaidi.
Mama wa mtoto huyo, Sarah Mwasanga aliomba msaada wa jeshi la polisi
kufanya jitihada za haraka kuhakikisha mtoto wake anapatikana.
Watu wanaovuka bahari ya mediterranea kutoka Afrika kasakzini.(Picha:UNHCR)
Taarifa zilizotolewa leo na Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji
IOM z inasema, wahamiaji 90 wameripotiwa kufa maji baada ya boti
waliyokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama katika bahari mediteranea
pwani ya Libya. Patrick Newman na maelezo kamili .
Shirika hilo linasema wahamiaji wanaendelea kupoteza Maisha kila
uchao wajaribu kwenda kusaka mustakhbali bora. Kufuatia mkasa huo Bi
Olivia Headon ambaye ni mwakilishi wa IOM Libya akizungumza na wandishi
wa habari kwa njia ya simu mjini Genevia amesema.. (Sauti ya Olivia Headon) Watu wapatao 90 wamekufa maji wakati boti waliokuwa
wakisafiria kupinduka mapema hii leo ,miili ya wa watu 10 kati yao,
wawili wakiwa raia wa Libya na wanane kutoka Pakistan imeokolea pwani
ya Libya, wakati huohuo vikosi wa uokowaji vya Libya vimeripoti kuokoa
watu wawili walioweza kuogelea hadi nchi kavu na mmoja kuokolewa na
wavuvi bahari.
Kwa mujibu wa ripoti ya IOM ya mwaka jana zaidi ya wananchi 29 wa
Libya waliripotiwa kuokolewa wakijaribu kwenda kusaka hifadhi
ughaibuni.
Halikadhalika wasaka hifadhi elfu tatu kutoka Pakistan wameripotiwa
kuingia Italia kupitia Libya mwaka 2017, ikilinganishwa na 240 katika
mwezi wa januari 2018 .
Baba wa
mabinti watatu waliodhalilishwa kingono na Daktari wa Mazoezi wa
Marekani, Larry Nassar amejaribu kumshambulia mbele ya mahakama ya
Michigan, baada ya kumvaa mshtakiwa huyo anayetuhumiwa kudhalilisha
wachezaji kadhaa waliopitia mikononi mwake. Hata hivyo Randall Margraves
hakufanikisha lengo lake hilo baada ya kudhibitiwa vyema na maofisa
watatu wa mahakamani hapo. Kabla ya kuvamia meza ya mshtakiwa Nassar,
mwanaume huyo aliomba kupewa “dakika tano ili afungiwe na shetani huyo” Jaji Janice Cunningham akasema hawezi kuruhusu jambo hilo. Lakini Margraves aliendelea kusisitiza
apewe dakika moja na kusababisha vicheko vya chini chini kutoka chumba
cha mahakama. Nassar, aliyewahi kuwa Daktari wa mazoezi wa Timu ya
Olympiki ya Marekani, alishahukumiwa miaka 175 jela wiki iliyopita baada
ya kutolewa ushahidi wa takribani waathirika 160 waliofanyiwa vitendo
vya udhalilishaji kingono. Akiwakilisha hukumu hiyo, Jaji Rosemarie Aquilina alimwambia Nassar: ” wewe hustahili kuonekana tena nje ya jela.” Waathirika wengi ni wale waliochukuliwa
kwaajili ya kutibiwa naye katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan,
alipokuwa akifanya kazi kama Daktari wa michezo.
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameviomba vyama vya
Chadema na CCM kusimamisha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na
udiwani kwa siku tatu kuomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe, Kingunge
Ngombale Mwiru.
"Kingunge amesaidia kuimarisha CCM na baadaye akasaidia Chadema. Sioni
busara vyama kuendelea na kampeni. Nawaomba wasitishe leo, kesho na
Jumatatu mwanasiasa huyu akizikwa wataendelea," amesema Zitto leo
Februari 3, 2018 akiwa katika msiba wa mwanasiasa huyo, nyumbani kwake
Kijitonyama, Dar es Salaam.
Vyama takriban 12 vipo katika kampeni za ubunge jimbo la Kinondoni
jijini Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro. Kampeni hizo zilianza
Januari 21 na kutarajiwa kumalizika Februari 16. Uchaguzi katika majimbo
hayo na Kata 10 utafanyika Februari 17, 2018.
Kingunge aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane, Oktoba 4, 2015
alitangaza kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote
lakini mara kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi
aliyekuwa mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa kwenye
uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Mwanasiasa huyo alifariki dunia jana Februari 2, 2018 katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Februari 5, 2018
katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Wakati Zitto akieleza hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na
Utawala Bora ), George Mkuchika amesema atamkumbuka Kingunge kwa
mengi.
Amesema alimfahamu Kingunge miaka ya 1970 wakati akiwa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, kwamba mwanasiasa huyo mkongwe alikuwa akienda kutoa
mihadhara wakati huo wakiwa wanachama wa Tanu.
“Kifo chake kimenistusha kutokana na mchango wake mkubwa wa kuunganisha vijana,” amesema Mkuchika.
BAADA ya gazeti hili kuandika habari yake kwa mara ya kwanza akiomba
msaada wa matibabu ya mguu wake, hatimaye staa wa filamu Bongo, Wastara
Juma amekamilisha kiasi cha shilingi milioni 37 alizokuwa akihitaji na
kesho (Jumapili) anatarajia kuondoka nchini kuelekea kwenye Hospitali ya
Sefaree iliyopo India kwa matibabu.
Wastara alisema kuwa, hakutarajia muitikio mkubwa wa kuchangiwa fedha
hizo na anawashukuru wote waliofanikisha kupatikana kwa msaada huo.
“Niwashukuru Watanzania wote kwa kunichangia, nimshukuru Rais Magufuli
na mkewe mama Janeth lakini kwa kipekee kabisa naomba nilishukuru gazeti
lenu (Risasi Jumamosi) kwa kuwafanya watu wengine wajue nina tatizo
gani na nahitaji msaada, bila nyie huenda mpaka leo ningekuwa nalia
kitandani, asanteni na Mungu awabariki,” alisema Wastara.
Wastara pia ameishukuru Global TV Online ambayo ilirusha sauti yake na video ikionesha jinsi alivyokuwa akipata maumivu.
Rais Magufuli, kutunuku kamisheni maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Watakaotunukiwa kamisheni ni maafisa wapya wa Tanzania na kutoka nchi
marafiki 197 waliopata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi
Monduli mkoani Arusha.
Rais Magufuli ameanza kwa kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri zaidi katika mafunzo hayo. Miongoni mwao ni pamoja na mwanafunzi aliyefanya vizuri katika medani zote.
Akifuatiwa na aliyefanya vizuri darasa.
Aliyefanya vizuri zaidi katika wanafunzi wote. Aliyefanya vizuri kwa wanafunzi wa kigeni, Mkundane Beka
Serikali
imesema mradi wa uchimbaji mafuta katika Kisima kilichoanishwa
kuchimbwa kwenye eneo la kijiji cha Ipera Asilia, kwenye hifadhi tengefu
ya bonde la Kilombero, mkoani Morogoro, unatarajiwa kuanza rasmi mwezi
Septemba, 2018 ambapo kisima hicho kinakadiriwa kuwa na mafuta kuanzia
lita milioni 180 hadi 200.
Akizungumza
jana Februari 2, 2018 katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao
cha nne cha mkutano wa 10 wa Bunge mjini Dodoma, Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani amesema kinachosubiriwa ni kibali kutoka Baraza la
Mazingira nchini (NEMC) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania
(TAWA), ili uchimbaji huo uanze rasmi.
“Mkataba
ulishasainiwa tangu mwaka 2012 kilihobaki ni utekelezaji wa uchimbaji
na ugunduzi wa mafuta, mafuta yanayotarajiwa kuchimbwa kwenye eneo hilo
yanafikia milionii 180 hadi 200, mtaji ni mkubwa na utakua na manufaa
kwa wananchi wako na nchi kwa ujumla,” alisema na kuongeza.
“Kinachosubiriwa
ni kibali cha mazingira kutoka NEMC na mamlaka ya TAWA, mwezi Julai
mwaka huu tumehakikishiwa mkataba utapatikana na Septemba uchimbaji
utaanza rasmi.”
Serikali
kupitia shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) liliingia mkataba wa
utafiti na uchimbaji wa gesi na uvunaji mafuta na Kampuni ya Mafuta na
gesi ya Swala (Swala Oil), ambapo katika utekelezaji wa mkataba huo
iligundulika kuwepo kwa wingi mafuta ya petrol na gesi katika vijiji vya
Mtimbira.
Leo February 2, 2018 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria msiba wa Rubani wa Ndege za Serikali, Marehemu Kapteni Dominic Bomani aliyefariki jana kwa ajali ya ndege kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume.