Jumatano, 28 Juni 2017

Nchi 33 kushiriki maonesho ya sabasaba yanayoanza kesho

 

 Nchi 33 pamoja na taasisi na kampuni zaidi ya 2800 zimethbitisha kushirikimaonesho ya 41 biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama sabasaba yatakayoanza kesho jijini Dar es Salaam katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema katika maonesho ya mwaka huu kumekuwa na maboresho kadhaa ikiwemo kufungwa Camera maalum za ulinzi.

Mmoja kati ya washiriki wa maonesho hayo kutoka wizara ya fedha na mipango ambaye ni msemaji wa wizara hiyo Ben Mwaipaja amesema wizara hiyo na taasisi zilizo chini yake zimepanga kuyatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa jamii.

News Alert: Rais wa TFF na katibu wake wakamatwa



 Taarifa iliyotufikia asubuhi hii inaeleza kuwa, Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao. hilo limethibitisha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia.

Mapacha wafa maji, mama ajitupa baharini siku ya Eid



 MAPACHA wawili waliokuwa wakiishi kata ya Kashai katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera walikufa maji juzi kwenye ufukwe za Ziwa Victoria wakati wakiogelea kusherehekea Eid, katika siku ambayo mama mmoja alijitupa baharini kutoka kwenye pantoni Feri, jijini Dar es Salaam kwa wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Agustino Ollomi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Ulomi alisema juzi majira ya saa 11:30 jioni, mapacha hao walikuwa wakiogelea ziwani katika eneo la Kiloyela lililopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani humo.

Marehemu mapacha hao walitajwa kuwa ni Hussein Hamis (12) na Hassan Hamis(12), na kwamba walikuwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kashai.

“Watoto hao walikuwa wa askari mwenzetu(wa) kitengo cha Usalama Barabarani," alisema Kamanda Ollomi na kwamba "walikuwa wakisoma darasa la saba.”
Alisema sababu ya kifo cha marehemu hao ni kuzidiwa na nguvu ya maji na kupelekea kuzama ambapo waliopolewa wakiwa wamefariki.

"Watoto wenzao baada ya kuona wenzao wakiendelea kuzama walipiga kelele ili kuomba msaada, lakini jitihada za kuwaokoa wakiwa hai zilishindikana," alisema.

"Tayari watoto hawa wamezikwa Juni 27 mwaka huu (jana) katika makaburi ya Kishenge, yaliyoko katika Manispaa ya Bukoba.

“Tunaendelea kuwasihi wazazi, kuendelea kuangalia usalama wa watoto wao hasa katika siku za sikukuu ili kuepusha madhara kama haya."

Jijini Dar es Salaam, mwanamke aitwaye Asha Yahya(30), mkazi wa Zanzibar anadaiwa kujirusha baharini akiwa katika kivuko cha MV Magogoni kwa lengo la kujiua, lakini wananchi waliwahi kumuokoa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke, Andrew Satta alisema tukio hilo lilitokea majira ya 2:10 asubuhi wakati akitokea Kigamboni kuelekea Ilala na kwamba sababu za kutaka kujiua ni wivu wa kimapenzi.

"Baada ya kumhoji alituambia kwamba sababu ya kutaka kujiua, eti mume wake anataka kuoa mwanamke mwingine," alisema Satta.

Katika tukio jingine katika kipindi cha sikukuu, Jeshi la Polisi jana liliokota mwili wa mtumishi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Masoud Abdulrahman(27) katika ufukwe wa Kisiwa cha Mbutu, kilichopo Kigamboni.

Kamanda Satta alisema marehemu kabla ya kukutwa na umauti huo alikuwa na wafanyakazi wenzake 20 ambao walikwenda katika ufukwe huo kwa ajili ya kufurahia sikukuu ya Eid, lakini wakati wakiogelea wimbi kubwa la maji liliwapiga na hivyo wote kupotea.

Alisema hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kufanya msako baada ya kugundua kwamba kuna watu waliosombwa na maji, waliwapata wenzake 20 ambao waliokolewa na kukimbizwa hospitali.

Kwa upande wa mkoa wa kipolisi wa Ilala, mtu mmoja ambaye jina lake halikujulikana mara moja aligongwa na basi la mwendokasi katika Barabara ya Uhuru na kufariki papohapo juzi pia.

Kamanda wa Polisi wa Ilala, Salum Hamdani, alisema mtu huyo aligongwa na gari hilo baada ya kuingilia barabara ya mwendokasi na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kibiti: Wawili wauawa kwa kupigwa risasi



 Kibiti. Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo (Jumatano).

Waliouawa wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.

Habari za awali zinaeleza maiti ya mwenyekiti huyo wa kitongoji bado haijaonekana na nyumba zao zimechomwa moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amekiri kutokea kwa mauaji hayo.

Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi.
chanzo na muungwana blog

je wajua?: Ndege kubwa kuwahi kutengenezwa duniani ingia hapa

Ndege ni chombo cha usafiri unaotumika kusafirisha au kwa ajili ya shughuli mbalimbali kutumia anga. Ikiwemo vita, fahamu ndege kumi zilizowahi kutumika katika vita kuu ya kwanza ya dunia na vita ya pili kuu ya dunia.


 



Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia ilikuwa Zeppelin-Staaken R.VI, ndege ambayo ilizifanya ndege za wakati huo zionekane kama mifano tu ya ndege. (Picha: San Diego Air and Space Museum)


Ndege nyingine kubwa kutoka Ujerumani ilikuwa Dornier Do X, ilifanana na meli na ilikuwa injini 12. Iliweza kubeba abiria hadi 100. Ilikuwa na uzani wa tani 56. (Picha: Bundesarchiv)



ANT-20 iliyoundwa na Tupolev ilitumiwa kama chombo cha propaganda, ilikuwa na kituo cha redio, ukumbi wa sinema na chumba cha kutoleshea picha. Ilikuwa na injini kubwa juu ya mgongo wa ndege kuiwezesha kupaa. (Picha: Wikimedia Commons)


Ndege kubwa zaidi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ilikuwa B-29 iliyoundwa na Boeing. Ndiyo iliyoangusha mabomu ya atomiki Japan. Ilifungua ukurasa mpya wa ndege za kuangusha mabomu za kusafiri masafa marefu.

 H-4 Hercules iliyoundwa na Howard Hughes ina mabawa marefu zaidi duniani kuliko ndege nyingine yoyote. Hata hivyo ilipaa angani mara chache tu.

 Convair B-36 Peacemaker ilikuwa ndege ya kwanza duniani ya kuangusha mabomu kuweza kusafiri kutoka bara moja hadi bara jingine. Ilitumiwa injini kadha za jeti na rafadha kadha kuweza kupaa. (Picha: Clemens Vaster)

B-52 Stratofortress iliyoundwa na Boeing inasalia kuwa moja ya ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani. Ilitumia injini nane kubwa. (Picha: Getty Images)


 Tu-160 ya Tupolev ingeweza kubeba jumla ya tani 275 ikipaa, na ilikuwa na mabawa makubwa zaidi yaliyoweza kujipinda kuwahi kuundwa.



Ingawa Boeing 747 ilikuwa ndege ya kwanza kuitwa Jumbo Jet, A380 ya Airbus ni kubwa kuliko Boeing 747. Ndege hii inaweza kuwabeba watu 850.


Ndege kubwa zaidi kuwahi kuundwa duniani ni An-225 ya Antonov ambayo ina injini sita na urefu wake ni mita 84. Ndege hii ina uwezo wa kubeba karibu tani 250

chanzo cha habari mitandao mbalimbali.

Kampuni ya Google yapigwa faini ya dola bilioni 2.7



 Google imepigwa faini ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kudai kuwa kampuni hiyo ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.


Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara.
Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi.
Kampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa.
Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo.
“Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU,” alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU.
Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya bioshara ya Google tangu mwaka 2010
Mbunifu wa Android azindua simu mpya
Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni.

chanzo bongo 5

Mazishi ya walioungua yafanyika Pakistan

Mlipuko huo unatajwa kuwa mkubwa zaidi kwa siku za karibuni nchini humo


Mazishi ya pamoja yamefanyika Pakistan baada ya watu 120 kufariki katika ajali ya moto uliolipuka kutokana na kusuka kwa mpira wa mafuta siku ya Jumapili.
Maombi kwa waliojeruhiwa yalifanyika na kwa waliozikwa pia.
Ulinzi uliimarishwa wakati wa mazishi huku watu hao wakizikwa katika makaburi sita ya pamoja yaliyochimbwa katika kijiji cha Bahawalpur.
Waliozikwa katika makaburi hayo ya pamoja ni wale ambao hawakuweza kufahamika kutokana na kuungua vibaya.
Vipimo zaidi vimechukuliwa na iwapo vitaendana na vya ndugu waliopoteza wapendwa wao wahusika watachukua mwili na kwenda kuuzika tena.
CHANZO BBC.

Marekani yachunguza shambulio kubwa la mtandao

Serikali ya Ukraine iliweka aina hii ya uvamizi wa mtandao uliofanywa hivi karibuni

Mamlaka nchini Marekani imesema inachunguza shambulio kubwa la kimtandao ambalo limekumba mifumo ya kompyuta duniani kote.
Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.
Mashirika mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, idara za serikali, makampuni makubwa, na kampuni za usafirishaji ni miongoni mwa zilizoathirika.


Siku za hivi karibuni uvamizi wa mitandao umeshika kasi duniani
Watumiaji wameambiwa komputa zao zimenasa mpaka walipe kiasi cha dola mia tatu katika akaunti isiyofahamika.
Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imewashauri watu wasilipe fedha hizo.
Huku ikisema hakuna uhakika kwamba, mafaili yaliyofungwa yatafunguka baada ya malipo hayo kufanyika.
Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na linaendelea sehemu nyengine duniani.

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeshindwa kupata ushindi katika game ya pili ya #COSAFACup2017 vs Angola FT 0-0



Michuano ya COSAFA 2017 bado inaendelea nchini Afrika Kusini kwa michezo ya Kundi A lenye timu za Tanzania, Angola, Mauritius na Malawi kucheza michezo yao ya pili jana.
Tanzania jana imecheza dhidi ya Angola wakati Malawi ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Tanzania kwa magoli 2-0, imecheza dhidi ya Mauritius ambayo pia ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Angola huku staa wa Tanzania Mzamiru Yassin akiibuka mchezaji bora wa mechi kati ya Tanzania na Angola.
Katika michezo ya jana Tanzania ililazimishwa sare na Angola huku pia Malawi na Mauritius zimemaliza dakika 90 bila kufungana. Kwa matokeo hayo Tanzania bado inaendelea kuongoza Kundi A kwa kuwa na point nne sawa na Angola ila anaongoza kwa tofauti ya magoli. Katika michuano hii timu vinara wa makundi ndio watafuzu kucheza robo fainali.

 

Jumanne, 27 Juni 2017

Lowassa ahojiwa masaa manne: Kabla ya kuachiwa kwa dhamana




Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa

 Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa kwa saa manne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo jijini Dar es salaam.



Akizungumza na waandishi wa Habari mapema baada ya mahojiano hayo Mwanasheria wa Chama cha

Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Peter Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena Alhamisi ya wiki hii saa 6.00 mchana.
Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,” amesema Kibatala.

Mourinho awasili Ureno kwa mazishi ya baba yake mzazi




Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho tayari ameshafika nchini Ureno kwa ajili ya mazishi ya baba yake mzazi.






Baba yake Mourinho aitwae Jose Manuel Mourinho Felix 79 amefariki Dunia wikiendi iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo huko jijini Setubal nchini Ureno.
Mapema jana Mourinho kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha ya baba yake huku ikiwa na rangi nyeusi na nyeupe (B&W) na hakuandika kitu huku maoni ya mashabiki wakionekana kumpa pole kwa msiba uliompata.
 Jose Mourinho is comforted by a friend following his father's passing on SundayThe group attended a church service ahead of Felix's funeral on Tuesday morning

MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI

 
images
 
 
 
 

Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania alilipia VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza kugawiwa leo kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria. Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%), 
Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo.
Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa  hii tayari imeshaainishwa.
Wizara inawakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini. 
Aidha, Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini. 
Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu  Afya
26 June 2017

Nje ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi baada ya Lowassa kuripoti




Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA na Waziri Mkuu wa zamani,  Edward Lowassa jana June 26 2017 alipata wito kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Asubuhi ya leo June 27, 2017 majira ya Saa nne Lowassa amefika kuitikia wito huo na hii ni hali ya ulinzi ulivyo nje ya Makao Makuu ya Jeshi hilo.



chanzo millardayo blog.