Alhamisi, 7 Juni 2018

Wavuvi 109 wamekamatwa nchini Kenya

Leo June 7, 2018 Jeshi la majini nchini Kenya limewakamata wavuvi 109 raia wa Tanzania kwa kosa la kufanya shughuli za uvuvi kwenye mipaka ya Kenya katika bahari ya Hindi kinyume na sheria.
Wavuvi hao walikamatwa katika kijiji cha Shimoni kilichopo kusini mwa Kenya karibu na mpaka wa Tanzania na kufikishwa katika mahakama ya Kwale June 3. Aidha wavuvi hao walishindwa kujiwekea dhamana ya zaidi ya shilingi laki nne za kitanzania kwa kila mmoja.
Kwa upande mwingine Mbunge wa Lunga Lunga, Khatibu Mwashetani amewateteta wavuvi hao na kuomba makamu wa rais  wa Kenya Ruto kuingilia sakata hilo ili kuzuia mgogoro wa kidiplomasia unaoweza kutokea.
Na mbunge huyo aliongeza kwa kusema kuwa wavuvi hao ni kama ndugu zao kwa sababu wanashirikiana katika mambo mengi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni