Jumatano, 6 Juni 2018

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja umeshuka kote duniani 2017 :UNCTAD




Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja-FDI  ulishuka mwaka wa 2017 kutoka  dola trilioni 1.87 mwaka wa 2016 hadi dola trilioni 1.43 mwaka wa 2017. Hii ikimaanisha kuwa uwekezaji huo ulishuka kwa asilimia 23.
Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya  kamati ya maendeleo na biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi.
Ripoti hiyo“Uwekezaji na sera mpya za viwanda “, imetathimini hali ya uwekezaji duniani katika  kipindi cha kati ya  2016 na 2017. Katibu Mkuu wa UNCTAD, Mukhisa Kituyi, amesema ushukaji wa FDI na pia kudorora kwa makampuni tanzu duniani vinaleta wasiwasi hususan katika nchi zinazochipukia kiuchumi
(SAUTI YA MUKHISA KITUYI)
“Ikiwa hakutafanyika juhudi za kuzuia mwenendo huu wa kupungua kwa uwekezaji wa makampuni makubwa  ya kigeni katika mataifa yanayochipukia  sanasana kwa miradi endelevu, matumaini yetu ya kuwa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja (FDI) utasaidia kusukuma gurudumu la kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 yatakuwamashakani.
 Ameongeza kuwa uwekezaji utahijika mno.
uwekezaji katika sekta ya uzalishaji utahitajika mno ili kuweza  kufanikisha  maendeleo endelevu katika nchi maskini. 
Ripoti inasema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mataifa mengi yamebadilisha sera zake za kiviwanda na kutoa mfano wa Marekani ambapo  mabadiliko katika mfumo wake wa kodi, “unaweza kuathiri mpangilio wa uwekezaji duniani.” Na hiyo ni moja ya sababu kubwa za kuporomoka kwa uwekezaji wa kigeni.
Ripoti inatoa sababu zingine   zinatokana na  kupungua kwa asilimia 22 ya  thamani ya ubia wa makampuni yanayopatikana  katika nchi tofauti na pia ununuzi  wa makampuni hayo.
Isitoshe thamani ya uwekezaji wa kampuni tanzu ambazo zinatoa mwelekeo  utakavyokuwa hapo baadaye  nayo ilishuka kwa kiwango cha asilimia 40.
 Ripoti hiyo ya UNCTAD imesema uwekezaji huo wa  FDI ndiyo muhimu wa kifedha  kwa uchumi wa nchi nyingi zinazoendelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni