Ijumaa, 8 Juni 2018

Tanzania imeshuka katika viwango vya FIFA

Bado zimesalia siku 6 fainali za Kombe la Dunia 2018  nchini Urusi zianze, shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limetoa viwango vya soka vya mwisho wa mwezi kwa timu zote wanachama.
Tanzania pamoja na kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DRC, imeshuka katika viwango hivyo vya soka kwa nafasi tatu kutoka 137 hadi nafasi ya 140.
Ujerumani wao wapo nafasi ya kwanza kama kawaida wakifuatiwa na Brazil waliyopo nafasi ya pili wakati Ubelgji wao wakiendelea kushika nafasi ya tatu, huku Senegal ndio taifa pekee la Afrika lililopo nafasi ya juu ikishika nafasi ya 27.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni