Mshambuliaji
Mohammed Rashid anatarajia kuanza kuichezea Simba katika michuano ya
SportPesa Super Cup inayoanza keshokutwa mjini Nakuru, Kenya.
Mohammed amejiunga na Simba akitokea Prisons na taarifa zinaeleza kwamba amemalizana na Simba jana usiku.
“Kweli wamemalizana na yeye sasa ni safari ya kwenda Kenya kwa ajili ya michuano ya SportsPesa,” kilieleza chanzo.
Hivi karibuni mshambuliaji huyo alikataa kuongeza mkataba na Prisons ingawa hakuwa amesema anataka kufanya nini.
Taarifa
zinaeleza alikataa kuongeza mkataba mpya baada ya kukubaliana jambo na
Simba, hivyo alikuwa akisubiri kumalizika kwa msimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni