Jumamosi, 2 Juni 2018

SIMBA TISA WAUAWA KIKATILI MARA:

Image may contain: dog and outdoorWananchi wa Kijiji cha Nyichoka wilayani Serengeti mkoani Mara wanadaiwa kuwaua Simba tisa kwa sumu kali huku mmoja kati yao akikatwa miguu,mkia na ngozi juu ya mgongo.
Tukio hilo limedaiwa kutokea jana jioni ambapo mpaka sasa inadaiwa kuwa simba 19 wameuawa kuanzia mwaka 2015 ambapo jumla ya simba saba waliuawa kwa sumu huku mwaka 2017, Simba watatu wakiuawa kwa kuwapigwa risasi.
Kuuawa kwa Simba hao kunaelezwa ni hasara kwa Taifa kwani simba mmoja huweza kugharimu zaidi ya dola 10,000 katika biashara ya utalii kwa kutazamwa kwa zaidi ya miaka 10.
No automatic alt text available.Image may contain: plant, tree and outdoor

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni