Jumanne, 5 Juni 2018

Simba na Yanga wamepangwa Kundi moja Kagame Cup





 
Michuano ya club Bingwa Afrika Mashariki na kati imezinduliwa leo na kutangazwa kwa ratiba kamili ya michuano hiyo, katibu mkuu wa chama cha soka Afrika Mashariki na kati CECAFA Nicolaos Musonye na Rais wa TFF Wallace Karia kwa pamoja wametangaza uwepo wa michuano hiyo 2018.
Ratiba ya michuano yote ya Kagame Cup

Michuano hiyo itachezwa kwa kutumia viwanja viwili vya Chamazi na uwanja wa Taifa, makundi yakiwa matatu na wapinzani wa jadi Simba na Yanga wamepangwa Kundi C na timu za St George ya Ethiopia na Dakadaha ya Somalia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni