Straika
wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunguka kuwa amejipanga
vizuri na jeshi lake kuhakikisha wanaibuka na ushindi mkubwa katika
mchezo wa kesho dhidi ya Team Kiba.
Samatta anacheza soka la kulipwa katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ameyasema hayo kuelekea katika mchezo wa kampeni maalum iliopewa jina la nifuate kwa ajili ya kuchangia elimu utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Mshambuliaji
huyo amesema kuwa wamejipanga vizuri yeye na timu yake kuhakikisha
wanaifunga Team Kiba katika mechi hiyo kutokana na maandalizi
waliyoyafanya.
“Tumejiandaa kwa mchezo wa kesho na tupo vizuri chini ya kocha wetu, Julio na jambo zuri ni kwamba tayari Kiba anajua kwamba tutawafunga mengi.
“Kikubwa ni kuwaomba Watanzania kujitokeza katika mchezo huo kwa sababu lengo ni kuchangia elimu ya wadogo zetu, hivyo watu wajitokeze kushuhudia burudani hiyo,” alisema Samatta.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni