Mbunge wa Ubungo Said Kubenea amelalamikia suala la Naibu spika Dkt.
Tulia Akson kukataa swali la mbunge wa Vunjo James Mbatia lisijibiwe
na waziri mkuu akieleza kuwa Naibu spika amekiuka taratibu za Bunge kwa
kupitisha maamuzi ambayo sio sahihi.
Akizungumza
na East Africa BreakFast ya East Africa Radio Kubenea amesema Dkt.
Akson ametaja sababu alizowahi kuzitoa Spika Ndugai jambo ambalo sio la
kweli kwa sababu Spika huyo alisema yeye kwa kupenda kuuliza maswala ya
dini kwa hivyo suala hilo halifanani na swali aliloulizwa waziri mkuu
hapo jana.
“Huu ni mwendelezo wa mamlaka za bunge kuporwa kwa maksudi na uongozi wa bunge kwani kanuni zinasema mbunge yeyote anayo haki ya kuhoji kwa waziri yeyote kuhusu mambo ya umma”, amesema Kubenea
Jana katika kipindi cha maswali na majibu Naibu Spika Dk. Tulia akson alikataa swali la James Mbatia lililohoji sababu za serikali kuwatumia barua baraza la maaskofu Tanzania KKKT ikiwataka waufute waraka walioutoa katika kipindi cha kwaresma.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni