Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kumbusu hadharani tena midomoni mwanamke mmoja anayeishi Korea kusini wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wake waishio nchini humo.
Tukio hilo lililozua utata lilitokea wakati Rais Duterte alipokuwa akizungumza na umati wa raia wa Ufilipino wanaofanya kazi nchi za nje (Diaspora) huko jijini Seoul.
Inadaiwa kuwa tukio hilo lilianza kama sinema baada ya kiongozi huyo asiyeisha vituko kumwita mwanamke wa kwanza na kumkumbatia na kisha kumbusu shavuni kabla ya kumwita huyo wa pili na kumtaka ambusu midomoni.
Katika tukio hilo
inadaiwa kuwa kwanza mwanamke huyo alisita na kurudi nyuma kisha kutii
wito wa Rais Duterte kwa kukubali kumbusu midomoni kiongozi huyo ambaye
amekuwa kwenye tuhuma nyingi za kuruhusu mauaji na udhalilishaji
wanawake nchini mwake.
Kundi la kutetea haki wa Wafilipino liitwalo Gabriela, limedai kuwa tukio hilo ni "maonyesho ya kuchukiza ya rais huyo.”
Hata hivyo baadaye mwanamke huyo alikaririwa akisema kuwa kitendo hicho "hakikuwa na uovu".
Kwa upande wake Rais Duterte mwisho wa hotuba yake alisema, tukio hilo lilikuwa ni kama burudani kwa ajili ya umati huo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni