Jumanne, 5 Juni 2018

Lissu Operesheni yake ya Mwisho yamalizika salama Jana


Operesheni ya mwisho ya Tundu Lissu imefanyika na kumalizika salama, Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), alifanyiwa operesheni jana, Juni 4,2018 ya kuunga mguu wa kulia.

 Operesheni hiyo ambayo ilifanyika katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji, Lissu aliizungumzia akasema itakuchukua takriabani saa 8 hivyo kuwaomba Watanzania kumwombea.

Saa 3 usiku jana Juni 4,2018, Mke wake, Alicia aliongea na kituo kimoja cha Habari kutoka Ubelgiji kuwa operesheni imemalizika salama.

"Namshukuru Mungu kwani operation ya 20 iliyokuwa ya masaa 8 imekwenda vizuri na amezinduka. As always he is stable. Asanteni sana," amesema Alicia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni