Jumatano, 6 Juni 2018

POLISI YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI

Image result for polisi tz image






 Jeshi la Polisi limewaonya wananchi kuhusu ukiukwaji wa sheria unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia ujumbe mfupi wa maandishi katika simu wakidai kutumiwa fedha, kuwasiliana na mganga fulani ama kushinda bahati nasibu.
Jeshi la Polisi, kupitia taarifa yake iliyoitoa leo, Jumatano limewatahadharisha wananchi kupuuza jumbe hizo pamoja simu wanazopigiwa kwani zina nia ovu ya kutaka kuwatapeli.
Katika Taarifa hiyo, Jeshi la polisi limesema kwa yeyote atakayepata usumbufu wa ujumbe au kupigiwa simu hizo aripoti polisi, na Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mitandao kinaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua.

Image may contain: text

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni