
Mgeni
Ramsi aliyefungua mafunzo ya WISN PLUS POA Dkt. Frank Jacob (katikati
waliokaa) ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika
picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mikoa ya Morogoro na
Dodoma yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA.
Mgeni
Ramsi aliyefungua mafunzo ya upangaji wa watumishi kwenye vituo vya
kutolea huduma za Afya kulingana na Uzito (WISN plus POA) kwa Mikoa ya
Arusha na Kilimanjaro Bw. Noel Kazimoto (katikati waliokaa) ambaye pia
ni Katibu Tawala Msaidizi kwa upande wa Serikali za Mitaa Mkoa wa
Morogoro, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo
yaliyofanyika katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA.
Bw. Renatus Mashauri ni mtoa mada ambaye pia ni Afisa Mwandamizi wa Rasilimali watu - mradi wa PS3
Happines Ndosi - Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji - Ifakara.
Solomon Daktari Kibaha, Mtoa mada.
Mratibu wa Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta ya Umma (PS3) Mkoa wa Morogoro Bw. David Laput.
Picha
mbili za juu ni baadhi ya wataalamu wa Sekta ya Afya walioshiriki
mafunzo ya WISN na POA yaliyoratibiwa na kufadhiriwa na PS3 na kufanyika
katika ukumbi wa ICE katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA
Mjini Morogoro.
Baadhi
ya timu ya viongoi wa mafunzo ya WISN PLUS POA wakiwa tayari kukabidhi
vitabu vilivyoandaliwa kwa ajili ya kutekeleza kile walichojifunza
washiriki wa mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Gracian Makota, Renatus
Mashauri na Bw. Sebastian Masanja. Wengine ni wenyekiti wa washiriki
wakati wa mafunzo na David Laput Mratibu wa PS 3 Mkoa wa Morogoro.
Bw.
Sebastian Masanja ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya
Utawala, Mkoa wa Kilimanjaro aliyefunga mafunzo hayo akimkabidhi vitabu
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya WISN PLUS POA SUA Mkoani Morogoro. Na Andrew Chimesela, Morogoro.Mafunzo
ya kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo unaojulikana kwa
jina la kitaalamu Workload Indicators of Staffing Needs - WISN na
Prioritaization and Optimization analysis – POA (WISN plus POA)
yaliyoanza Juni 4 mwaka huu na kufanyika katika ukumbi wa ICE wa Chuo
Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne – SUA Mkoani Morogoro yamehitimishwa Juni 8
kwa mafanikio makubwa.Akiongea
na washiriki wenzake wakati wa Kufunga mafunzo hayo Katibu Tawala
Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Kilimanjaro Bw.
Sebastian Masanja amewapongeza wakufunzi wa mafunzo hayo kwa kujitahidi
kuwapa kile walicholenga kutoa hadi wao kuelewa kwa ufanisi na kwa niaba
ya wenzake ameahidi kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika
Halmashauri zao.Bw. Masanja
ambaye alikuwa mgeni rasimi katika kufunga mafunzo hayo amewataka
washiriki wenzake kutambua kuwa hadi sasa watumishi wa Serikali hususan
wa kada ya Afya bado hawatoshelezi kwenye vituo vya kutolea huduma,
hivyo ni wajibu wao kutumia mafunzo waliyoyapata kuisaidia Serikali
kuwapanga vizuri watumishi waliopo kulingana na uzinto wa kazi.“Washiriki
wenzangu, tumeshajifunza kuwa kituo cha Afya kilichopo Mjini hakiwezi
kulingana majukumu yake na uzito wake wa kazi na kituo cha Afya cha
kijijini, kwa sababu hata idadi ya wagonjwa inatofautiana, kwa hiyo
tuisaidie Serikali kuondoa malalamiko kwa kuwapanga vizuri watumishi
waliopo kulingana na uzito wa kazi zinazopatikana kwenye maeneo husika”
alisema Bw. Masanja.Mafunzo hayo
yalilenga kuimarisha upangaji wa watumishi kwenye vituo vya kutolea
huduma za Afya kulingana na Uzito wa kazi, kwa kutumia Mfumo wa
kisayansi wa WISN PLUS POA na kushirikisha Wataalamu wa Sekta ya Afya
kutoka Mikoa minne ambayo kwa kituo cha Mkoa wa Morogoro kilijumuisha
Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro na Arusha.Haya
ni mafunzo yanayofadhiriwa na Mradi wa uimarishaji mifumo katika Sekta
ya Umma (Public Sector System Strenthening - PS3) na kuratibiwa na Ofisi
ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, wawakilishi kutoka Halmashauri na taasisi ya Touch Foundation
na yanatolewa kwa Wataalamu wa sekta ya Afya kwa Halmashauri za mikoa
yote 26 ya Tanzania Bara.
Mafunzo
ya kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo unaojulikana kwa jina la
kitaalamu Workload Indicators of Staffing Needs - WISN na Prioritaization
and Optimization analysis – POA (WISN plus POA) yaliyoanza Juni 4
mwaka huu na kufanyika katika ukumbi wa ICE wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoinne – SUA Mkoani Morogoro yamehitimishwa
Juni 8 kwa mafanikio makubwa.
Akiongea
na washiriki wenzake wakati wa Kufunga mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi
Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu
Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja amewapongeza wakufunzi wa mafunzo
hayo kwa kujitahidi kuwapa kile walicholenga kutoa hadi wao kuelewa kwa ufanisi na kwa niaba ya wenzake ameahidi kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika
Halmashauri zao.
Bw.
Masanja ambaye alikuwa mgeni rasimi katika kufunga mafunzo hayo amewataka
washiriki wenzake kutambua kuwa hadi sasa watumishi wa Serikali hususan wa kada
ya Afya bado hawatoshelezi kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo ni wajibu wao
kutumia mafunzo waliyoyapata kuisaidia Serikali kuwapanga vizuri watumishi
waliopo kulingana na uzinto wa kazi.
“Washiriki
wenzangu, tumeshajifunza kuwa kituo cha Afya kilichopo Mjini hakiwezi kulingana
majukumu yake na uzito wake wa kazi na kituo cha Afya cha kijijini, kwa sababu
hata idadi ya wagonjwa inatofautiana, kwa hiyo tuisaidie Serikali kuondoa
malalamiko kwa kuwapanga vizuri watumishi
waliopo kulingana na uzito wa kazi zinazopatikana kwenye maeneo husika” alisema
Bw. Masanja.
Mafunzo
hayo yalilenga kuimarisha upangaji wa watumishi kwenye vituo vya kutolea huduma
za Afya kulingana na Uzito wa kazi, kwa kutumia Mfumo wa kisayansi wa WISN PLUS POA na kushirikisha Wataalamu
wa Sekta ya Afya kutoka Mikoa minne ambayo kwa kituo cha Mkoa wa Morogoro kilijumuisha
Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro
na Arusha.
Haya
ni mafunzo yanayofadhiriwa na Mradi wa uimarishaji mifumo katika Sekta
ya Umma (Public Sector System Strenthening - PS3) na kuratibiwa na Ofisi ya Rais -
TAMISEMI, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
wawakilishi kutoka Halmashauri na taasisi ya Touch Foundation na yanatolewa kwa Wataalamu wa sekta ya Afya kwa
Halmashauri za mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni