Alhamisi, 7 Juni 2018

KAGERE AIPELEKA GOR MAHIA FAINALI KUCHEZA NA SIMBA, SINGIDA YAAGA MASHINDANO




Singida United imeshindwa kufuzu kucheza fainali ya Super Cup nchini Kenya kwa kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Gor Mahia FC kwa mabao 2-0.

Meddie Kagere amekuwa shujaa wa mchezo huo kwa kufunga mabao yote mawili na kuiwezesha Gor Mahia kutinga hatua ya fainali.

Baada ya ushindi huo, Gor Mahia imeungana na Simba kucheza fainali itakayopigwa Jumapili ya wiki hii.

Simba ilikuwa ya kwanza kufika fainali kwa ushindi wa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kwenda suluhu tasa ya 0-0 dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni