Nimeona nikae chini niipitie maandiko ya mhenga moja aliyeandika habari ya DISCO iliyokua na kichwa cha habari "WAHENGA TULITESA SANA ENZI ZETU DISCO LA MCHANA (BOOGIE) NA MA-DJ WAKALI!!!" mwandishi wa habari hiyo amejitahidi sana kuelezea kwa mapana ya ufahamu wake jinsi gani alivyoujua muziki wa Disco wa enzi zile waliwemo maDj wake.
Mimi
nimeamua kuweka sawa baadhi ya mambo Dj Kalikali yeye alishapiga muziki
YMCA wakishirikiana na Dj Niga Jay na kuna wakati pia walipiga pamoja
na Dj John Peter Pantalakisi na muda mwingi John Peter Pantalakis
walikua wakishirikiana na Dj Chogy Sly Dico la Born City na kuna kipindi
fulani Dj Kalikali alikua Dj wa Disco la RSVP ambalo Mbowe walianzisha
tawi la DICO katika hotel ya New Africa ghorofa ya saba.

Muziki
wa Disco unasafari ndefu maDj wengi wa zamani walikua wanamuziki wa
bendi na baadae kubadili mwelekeo na kuwa maDj kwa mfano Dj Sweet
Francis na Dj Addy Sally chimbuko lao walitokea kwenye bendi na baadae
miaka ya 1970 wakahamisha mawazo yao na kuwa maDj wakati huo kukiwa na
Disco la Banda Beach, Sea View na madisco mengine Kilimanjaro Hotel
Summit
Nataka
nikupe historia ya musiki na disco theque.Africana Gogo Disco lilianza
mwaka 1971 na aliyeanza kupiga disco hapo ni Bhoka Wilson (Mzimbabwe)
wakati ule ikiitwa Southern Rhodesia naye alikuwa cabbaret singer Simba
Grill Kilimanjaro hotel. August 1972 Dj Sweet Fransis akawa Dj hapo
mpaka Nov.1973 kisha akawa Dj. Judy Kingui (Msouth Africa ambaye alikuwa
mkewe Kingui aliyekuwa mwenye The Rifters Band. Judy alikuwa Dj.hapo
Gogo Disco mpaka 1975.
Katika historia ya muziki wa disco Tanzania ambayo inabeba Madj wengi wengine wakiwa wametangulia mbele ya haki
Disco la XTC ambalo maDj hawa wamepitia David , Lawrance , Pailonga, TNT Jackson
Disco la Valentinos/Continental haliwezi kutajwa bila ya watu hawa Ibrahim G ,Camal, Mr A, Salai, Meb, Guru, Sabry Kube
Disco la Rungwe 110 halijakamilika bila ya watu hawa Chogy Sly JP Pantelakis, Roma Pop Juice, Amon Washington, Agib Show, Ibony, Ntimizi, Bhester, Kim and the boyz, John Bure na wengineo

Dj
Sweet Francis jina kamaili ni Francis James Bundala,mwaka 1964
alianzisha bendi iliyoitwa The Screemers na Dj Sweet Francis akiwa
mwimbaji(singer) hapo ndipo alipopewa jina la SWEET baada ya kusikia
sauti yake na jinsi alivyokuwa akiimba iliwakuna sana na wakawa wanasema
"YOUR VOICE IS SO SWEET " na ndiyo hapa akawa anaitwa Sweet. Hiyo ni
hapa Dar.Bendi The Screamers ilidumu muda mfupi. Mwaka 1965 alianzish a
bendi nyingine ya watu 5 wakaiita The Hot Five wakawa wanapiga bugi kila
Jumapili mchana hapo Arnatoglo hall Mnazi mmoja. Wakawa wanashindana na
bendi ilikuwa inaitwa The Flamming Star.
Mwaka
1967 June The Hot Five ikavunjika. 1967 Sept. Dj Sweet Francis na
aliyekuwa Solo guitarist wakaanzisha bendi nyingine wakapata watu
wengine 3 ambao walianza kuwafundisha ambao walikuwa mpiga bass, mpiga
rythym na drummer. Bendi wakaiita The TONICS. Mwimbaji- Sweet, Solo-
Michael Jackson, Rythym- Green Jackson. Bass- John Morand na Drums-
Charles Alowasa.
Baada
ya mazoezi makali mwezi November1967 wakaapata mkataba wa kupiga muziki
kila siku hapo Splendid Hotel iliyokuwa inamilikiwa na mtaliano
aliyeitwa MOSKA mtaa wa Samora zamani ukiitwa Independence Ave.
Siku moja wakati wanapiga muziki jamaa mmoja ambaye hawakuwa na mazoea naye akaja kwenye stage akaomba apige bongos wakamruhusu, wakati Dj Sweet Francis anaimba na yule jamaa akawa amapiga bongos vizuri sana Dj Sweet Francis akawaambia wenzake kuwa anafaa kuwa drummer lakini wenzake walimkatalia na baada ya kuwasihi sana walikubali kwa sharti kuwa amfundishe kupiga drums mpaka ajue.

ya kumfundisha kwa muda mfupi akaona ameelewa na baada ya kumpa nafasi
kwenye stage alipiga drums na wenzangu wakamfurahia, huyo alikuwa
anaitwa Adam Salehe Mwambile (R.I.P.) na tangu siku hiyo Dj Swett
Francis akamwambia kuazia leo utaitwa ADDY SALLY, ilikuwa mwezi April
1968, hilo ndiyo lilikuwa chimbuko la ADDY SALLY.
May
1968 mkataba ulimalizika hapo Splendid wakaamua kwenda mikoani.Wakati
wote huo Dj Sweet Francis alikuwa mfanyakazi wa NPF sasa ni NSSF.
Dj Sweet Franacis aliamua kuacha kazi maana alivutiwa sana na muziki. July 1968 walifika Arusha wakiwa wanamuziki 5 na fundi mitambo aliyejulikana kwa jina Joseph Magali.
Dj Sweet Franacis aliamua kuacha kazi maana alivutiwa sana na muziki. July 1968 walifika Arusha wakiwa wanamuziki 5 na fundi mitambo aliyejulikana kwa jina Joseph Magali.
Yule
drummer wa kwanza .walimwacha baada ya kumwona Dj Addy Sally anafaa
zaidi. March 1970 Dj Sweet Francis walirudi Dar. May1970 Dj Sweet
Francis na Addy waliacha bendi kwa kutoelewana na Michael Jackson ambaye
ndiye aliyekuwa kiongozi wa Bendi.
July 1970 Dj Sweet Francis alienda Mombasa na kuanza kuimba na Sunshine club. Mwezi Sept.1970 Dj Sweet Francis alimwita Dj Addy Sally Mombas akawa anapiga drums Central night club, May 1971 wakarudi wote Dar.

Wakati
huo The Tonics wakiwa Nairobi waliwaita Dj Sweet Francis na Addy Sally
huko, Dj Sweet Francis alikataa ila Dj Addy Sally akaenda.
Dj Sweet Francis akawa anaimba mara moja moja Simba grill Kilimanjaro Hotel wakiwa na bendi kutoka Spain iliyoitwa Los Valdos na hotel ikiwa ya chini ya raia kutoka Israel aliyejulikana kwa jina la LEVY na meneja mkuu wa hotel akiitwa FERGUSON raia wa Canada.
Kwa vile Africana hotel ilijengwa kutokana na faida ya pesa za Kilimanjaro hotel hivyo mmiliki alikuwa mmoja na mwaka 1971 ilianzishwa Gogo Disco baada ya kuhamisha disco kutoka Summit, Kilimanjaro hotel kwenda Afrikana. Bokha Wilson alikuwa msanii wa Cabaret Simba grill pia kuwa Dj. Summit akahamishiwa Gogo disco hotel Africana. August 1972 Bokha Wilson akarudishwa Simba grill na Dj Sweet Francis akapelekwa Africana Hotel kuwa Disc Jockey Gogo Disco Theque.

Wote
waliotajwa hapo mwanzo wameshatangulia mbele ya haki isipokuwa Dj Sweet
Francis na Bhoka Wilson hatuna taarifa zake, miaka ya 80 alikuwa
Ujerumani. baada ya kuwa Dj wa Gogo disco.

Dj
Sweet Francis alipanda kwenye stage na kuanza kuimba, cha ajabu kila
mtu aliufurahia sana huo wimbo na walimshangilia sana na aliporudi
mezani kwake, yule jamaa ambaye hakumjua alisimama akampa mkono akasema "
Kumbe hapa tumekaa na mwanamuziki mzuri hivi, (akaendelea) Sikia kijana
mimi najenga hotel hapo mtaa wa Uhuru na karibu kumalizika, hivyo ikiwa
tayari wewe nataka uanze muziki hapo. Dj Sweet Francis akamkubalia,
Hotel ikawa tayari Nov.1979 na kabla ya Dj Sweet Francis hajajiunga na
Keys Hotel alipiga Disco kwa muda mfupi Mbowe Hotel na hapo ndipo
alipomfundisha Dj.Jerry Kotto na Dj Sweet Francis akaanza kupiga Disco
Keys Hotel Dec.1979.
Baada
ya Addy Sally kurudi toka Lusaka, mwezi April 1980 wakawa pamoja hapo
Keys Hotel akiwa vyombo vya Disco vipya kabisa vikiitwa M3. waliendelea
pamoja hapo Keys Hotel lakini kufika Dec.1980 Dj Sweet Francis
walishindwa kuelewana na Addy, ikabidi Addy aondoke.
Jan.1981
Dj Sweet Francis akawa na Dj. Seydou na baada ya muda kidogo Dj.Seydou
akaondoka baada ya mzee Ndesamburo (R.I.P) kununua vyombo vya Disco na
baada ya hapo Dj Sweet Francis akapiga Disco na Dj Johnson Pantaleo
(R.I.P) na ndiye Dj Sweet Francis aliyemuacha Keys hotel,
June 1981 ndio ukawa mwisho Dj Sweet Francis wa kupiga disco.

Mwezi
Sept.1981 Dj Sweet Francis alienda Ujerumani na nchi zingine za Ulaya,
alirudi Dar. Sept.1983 baada ya mapumziko 1993 Oct. akaanza tena kuwa
Cabaret singer hapo International Pub, Kijitonyama nyuma ya Sayansi na
Teknolojia mpaka June-August 1994. Sept 1994 Simba Grill Kilimanjaro
Hotel. Nov.2003--June 2004 Cine Club. Hii ndiyo historia yake katika
tasnia ya muziki. Mwanamuziki na Disc Jockey "SWEET FRANCIS."
Baada
ya kumalizana na hiyo historia ndefu na nzuri ya Dj Sweet Francis sasa
turudi tena kwenye historia ya Disco wakiwemo maDj wake.
Disco la Motel Villa pamoja na madj wengi kupitia hapa lakini dj maarufu wa hapo alikua Kim and The Boys ambaye pia kuna wakati alikua maarufu katika kupromoti madansa.
Disco la Motel Villa pamoja na madj wengi kupitia hapa lakini dj maarufu wa hapo alikua Kim and The Boys ambaye pia kuna wakati alikua maarufu katika kupromoti madansa.
Paul
Mc Ghee alianzia Morogoro akiwa na disco la Biribi likiwa chini ya
usimamizi wa kaka yake Joseph Kusaga anayeitwa Justine Kusaga. Baadae
Disco lilikua chini ya usimamizi wa Joe Kusaga nakubadilika jina na kua
Mawingu Dj alikua Paul Mc Ghee na baadae Disco lilihamia Dar likiwa
linapiga muziki wake Salender Bridge na ndio ukawa mwanzo wa kukua kwa
Disco hilo na kuendelea kupiga Motel Agip, Pool side hotel ya Kilianjaro
kila Jumapili, New Africa ghorofa ya Saba, Twiga na baadae wakaanzisha
Disco la Bolingo Tazara, na kuendelea kupanua wigo wao mpaka Arusha.
Clouds walikua na maDj wengi na Disco hili lilikuza vipaji, vijana wengi
wa enzi hizo wakiwemo Boni Luv, Stev B (R.I.P.), Rankim Ramadhani
(R.I.P.) na wengine wengi wakiwasaidia maDj Jesse Malongo, Dj Young Ray
akiwemo Joseph Kusaga mwenyewe.
Hapa ni baadhi ya maDj waliokua chini ya Joe Kusaga Dj
Jesse Malongo, Sterwat Chiduo (Dj Young Ray), Elliud Pemba, Dj Louis,
Ebonite Who jack, Julius Tandau, Julius Kagaruki, Boni. Luv, Stev B
(R.I.P.), Clouds Ma Dj
tulikuwa Elliude Pemba (Elliwood), Jesse Malongo (Babyface), Joseph
Kussaga (Emperor), Stuart Chiduo (Young Ray), Julius Tandau (Jet),
Richard Mazula (Ebonite woo Jack)
Elliud Pemba (Dj Elliwood) safari
yake ya muziki imeanzia Clouds pale Motel Agip Snack Bar, Kilimanjaro
Pool Side, Seventh Floor New Africa Hotel, Dar es Salaam Institute na
Twiga.
Dj Ellud Pemba ndio niliyemwachia Dj Boni luv U Dj mwaka 1992 baada ya kwenda Shule na 1994 Kuanza kazi nyingine ITV.
Dj Ellud Pemba ndio niliyemwachia Dj Boni luv U Dj mwaka 1992 baada ya kwenda Shule na 1994 Kuanza kazi nyingine ITV.
Disco
la Space 1900 wakati huo likiwa chini ya usimamizi Sudi Ally Salehe
lilianzia Mbowe chini ya maDJ Saydou na Gerry Kotto na Sudi Ally Salehe
walikua washirika na Dj Saydou walichangia vyombo vya muziki disco
pamoja.
chanzo michuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni