Jumanne, 22 Mei 2018

ZANZIBAR YAONYA WAFANYABIASHARA:



Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko imewataka wananchi wake kutoa taarifa pindi watakapouziwa bidhaa zinazotumika kwa ajili ya futari katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kwa bei ya juu mbali na ile elekezi iliyotolewa na serikali.
Akizungumzia suala hilo. Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Hassan Khamis Hafidhi amesema lazima wafanyabiashara watekeleze agizo la serikali la kushusha bei ya bidhaa hizo ikiwemo Mchele, Sukari, Unga wa ngano na Tende kwani tayari Serikali imewaondoshea kodi kwa bidhaa hizo wanapoingiza nchini.
Bei elekezi zilizopangwa na Serikali kwa bidhaa hizo ni pamoja na:
Sukari Kilo isizidi shilingi 1,700 kwa Zanzibar, na shilingi 1,800 kwa Pemba
Unga wa ngano kilo usizidi shilingi 1,100
Tende kilo shiilingi 3000
Mchele kilo shilingi 1,250
Hafidh amesema endapo wafanyabiashara hao watakaidi agizo hilo hatua za kisheria zitachukulia dhidi yao kwani watakuwa wamedhamiria kuwapa usumbufu wananchi ambao wanahitaji bidhaa hizo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni