akizungumza na mwandishi wa mwana wa liganga blogspot.com, H mwana amesema kuwa wasanii wakubwa nchini wanajisahau kusaidia wenzao wanao anza muziki na filamu kwani pasipokujua nao wametokea chini na kuweza kufahamika kupitia muziki na filamu.
msanii huyo ambaye anatamba na nyimbo ya kisambari , sir angel, ambapo pia ameweza kucheza filamu be care ful with women ambapo aliweza kushirikisha wakongwe wa filamu hapa nchini kama rose ndauka,ben branco maarufu kama beni na mzee magari, ameongeza kuwa Tanzania ina vipaji lukuki ambavyo vikitumiwa ipasavyo serikali inaweza kunufaika kama itatengeneza mazingira mazuri kwa wasanii.
''tanzania tumejaliwa vipaji lukuki kama serikali itatengeneza mazingira bora kwa wasanii wa muziki na filamu tungekuza uchumi kupitia tasnia hii''anasema H mwana.
msanii huyo ambaye maskani yake ni katika jimbo la mlimba mkoani morogoro anatoa wito kwa wadau na kusaidi wasanii wa chipukizi.
kwa upande wa maandalizi ya kazi zake mpya msanii huyo amesema anajipanga kuachia kazi zake mpya kwa upande wa muziki na filamu .''mashabiki wangu wakae mkao wakula kwani kuna filamu yangu mpya na ngoma mpya ambapo vitatoka hivi karibuni, kwasasa najiandaa kufanya uzinduzi wa kazi hizo '' alisema msanii huyo.
hapa H mwana anatoa wito kwa wasanii kuungana na kusaidiana kufanikisha ndoto zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni