Muimbaji huyo amesema baada ya kushinda tuzo ya BET watu walifikiri angebadili aina muziki wake lakini sivyo alivyo yeye.
“Watu walikuwa hawajaelewa, walikuwa wanafikiri tuzo zinafanana na muziki wa aina fulani lakini nyimbo zilizonifanya nichukue tuzo ni hizi hizi za nyumbani,” amesema.
“Hakuna nyimbo za kuchukulia tuzo, hizo za nyumbani, mimi nafanya muziki kwa ajili ya mashabiki zangu na watu wa Afrika Mashariki,” Rayvanny ameiambia Bongo5.
Soma Pia: Rayvanny aibuka shujaa kwenye BET
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni