Timu ya wasichana wanaoishi kwenye mazingira magumu kutoka Tanzania
imetinga fainali za Kombe la Dunia la Watoto baada ya kuifunga England
kwa mabao 2-1 kwenye mechi ya nusu fainali
Magoli ya Tanzania yamefungwa na mlinzi Mastura Fadhili na mshambuliaji Asha Omari.
Tanzania itacheza fainali na Brazil kesho kutwa, Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali goli 1-0.
Hadi inatinga fainali, Tanzania ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo, imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja tu.
Tanzania ilitwaa ubingwa wa kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2014 nchini Brazil.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni