Jumatatu, 14 Mei 2018

MACHINJIO YA KISASA MWANZA:



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Mkoa na Jiji la Mwanza kwa kuboresha machinjio ya Kisasa ndani ya jiji hilo.
Jafo ametoa pongezi hizo alipotembelea mradi huo mkubwa ambao mara baada ya kukamilika kwake kutawezesha kuchinjwa ng'ombe 700 kwa siku.
Aidha mradi huo unatarajiwa kuongeza mapato ya jiji hilo kutoka Shilingi milioni 30 kwa mwezi hadi Shilingi milioni 120 kwa mwezi.
Akizungumza katika mradi huo, Waziri Jafo amezitaka Halmashauri nyingine nchini kuiga utekelezaji wa mradi kama huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni