Polisi nchini Indonesia imeimarisha ulinzi katika makao makuu yake na maeneo mbalimbali nchini humo kufuatia washambuliaji wawili waliobeba mabomu kuyalipua wakitumia pikipiki katika mji wa Surabaya ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini humo na kujeruhi watu 10.
Milipuko hiyo imetokea siku moja tu baada ya mashambulio ya mabomu yaliyoua watu kumi na wanne katika maeneo tofauti ya makanisa na kujeruhi wengine 40 ambayo baadaye yalibainika kutekelezwa na familia moja.
Msemaji wa polisi katika eneo la Java Mashariki, Frans Barung Mangera
amesema mwanaume na mwanamke waliokuwa wamepanda pikipiki walisimama
kwenye eneo la ukaguzi kabla ya kulipua mabomu.
Mamlaka za Indonesia zimesema miongoni mwa watu waliojeruhiwa ni pamoja na raia sita na askari polisi wanne.
Rais wa Indonesia, Joko Widodo amesema mashambulio ya mabomu ya jana na leo yanafanywa na watu waoga.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni