Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli
amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya
Chuo cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College).
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi huo umeanza rasmi leo Mei 13.
Kabla ya uteuzi wa leo Prof Tumbo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha
zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (Center for Agriculture
Mechanization and Rural Technology - CAMARTEC).
Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mussa Iyombe kuwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa
Umma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni