Akikagua kituo hicho, Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile ameagiza maafisa wa uhamiaji kuhakikisha kwamba wasafiri wote wanaotumia uwanja huo wanapimwa. Aliongeza kuwa serikali pia imefungua kwenye uwanja huo zahanati maalum ya kutibu wasafiri watakaopatikana na Ebola.
“Tunajitahidi kuhakikisha kwamba ugonjwa huo hauingii nchini,” alisema Ndugulile. Ugonjwa wa Ebola uligunduliwa katika nchi jirani ya DRC ambapo tayari imeua watu 20.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni