Jumanne, 22 Mei 2018

PICHA TATU BORA ZILIZOCHAGULIWA NA MAHARUSI

Image may contain: 2 people, people smiling, wedding Maharusi Prince Harry na Meghan ambao walifunga ndoa mwishoni mwa wiki, wameruhusu picha tatu bora walizozichagua wao kama chaguo lao muhimu kwa siku hiyo.
Wawili hao walioana Jumamosi, Mei 19 katika harusi iliyoweka rekodi duniani kwa kuwa harusi ya mfano iliyovunja mipaka ya tamaduni na rangi na mila na tofauti nyingine, katika ujumbe wao ulioambatana na picha hizo wamesema, wanajiona na kujihisi wenye bahati kushiriki na watu takribani 120,000 waliomiminika kwenye mji wa Windsor na mamilioni waliofuatilia siku yao hiyo kuu ulimwenguni.
Picha hizo ambazo zimechaguliwa na wawili, miongoni mwao ni ile inamuonesha Meghan akiwa amekaa katikati ya miguu ya Harry katika kasri la Windsor huku mwana mfalme huyo akiwa na tabasamu kubwa mbele ya Kamera wakati bibi harusi akicheka na mtu mwingine upande wao wa kushoto.
Picha nyingine ni ile iliyomuonesha Malkia akiwa huru na kusahau nafasi yake hiyo kuu akiwa pamoja na mama yake Meghan Doria Ragland, mwenye miaka 62, akiwa amesimama na mwanaye sambamba na sehemu kubwa ya wanafamilia ya Kifalme.
Picha ya mwisho waliyoiruhusu wawili hao ni ile inayowaonesha watoto wa kaka yake Harry, Prince George na dada yake Princess Charlotte wakionesho kufurahia wakati waliojumuika na wasichana na wavula waliosimamia harusi ya Harry na Meghan ambaao wote wakionekana wenye furaha.
Picha za wawili hao zimepigwa na mpigapicha maarufu Alexi Lubomirski, 42, ambaye alikuwa ni mpigapicha wa mama yake Princess Diana.
 Image may contain: 19 people, people smiling, wedding and indoor











Image may contain: 12 people, people smiling, wedding

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni