Jumanne, 22 Mei 2018

MAUAJI YA KIMBARI RWANDA YASABABISHA BOMOA BOMOA

Image may contain: outdoor and nature



Image may contain: food
 Nyumba kadhaa nchini Rwanda zimelengwa kubomolewa katika zoezi la kutafuta makaburi ya halaiki mwezi mmoja baada ya makaburi mengine kadhaa kugunduliwa ya mabaki ya watu waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari mwaka 1994 huko Kabuga nje ya mji mkuu Kigali.
Kwa mujibu wa BBC, wahusika wa shughuli ya kufukua masalio ya miili ya watu waliouawa wanasema kwamba tayari wameshafukua masalia ya watu zaidi ya 400 na kwamba mashimo zaidi yanapatikana kila uchao.
Kutokana na hofu hiyo ya uwepo wa mashimo zaidi, maafisa wafuatiliaji wa ufukuaji huo wameamua kuendesha zoezi la bomoa bomoa litakalogusa nyumba zote zinazoshukiwa.
Inakadiriwa kwamba takriban watu 7000 walizikwa katika makaburi ya halaiki nchini.
Wakuu wa kitengo cha kupambana dhidi ya mauaji ya kimbari wanasema watawafidia wamiliki wa nyumba ambazo hazitakuwa na masalio ya miili ya watu baada ya ubomoaji huo.
“Tunapofukua tunapata mifupa midogo midogo sana, na nywele. Watu wengine walikatwa katwa kama nyama za ng'ombe. Pia tindikali iliteketeza kabisa mifupa ya vichwa kiasi kwamba ni vigumu kutambua kichwa kimoja'' alisema mkuu wa Jumuiya inayotetea maslahi ya manusura wa mauaji ya kimbari.
Nguo zilizochanika na kupatikana ndani ya makaburi hayo ya pamoja ndiyo ishara pekee inayotumiwa na watu kutambua jamaa zao kutokana na kwamba inachukua muda nguo kuharibika.
Shughuli hii ya kufukua makaburi haya ya pamoja huenda ikachukua muda mrefu kufuatia ukubwa wa maeneo yanayokisiwa kwamba kulizikwa watu mwaka 1994.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni